KIONGOZI MWINGINE WA ACT WAZALENDO ANG’ATUKA

Katibu wa Chama ACT-Wazalendo Mkoa wa Mbeya, Bahati Longopa ametangaza kung’atuka madarakani kwa kile alichodai kutoridhishwa na kitendo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Elisha Mghwira kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Longopa wakati anatoka kwenye wadhifa huo alisema haoni sababu ya kuendelea kuwa kiongozi wa chama hicho kwani kitampa wakati mgumu kuhamasisha wanachama wapya katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
Kiongozi huyo alisema hakubaliana na suala la Anna Mghwira kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiitumikia serikali ya awamu ya tano ambayo iko chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Nimeamua kwa hiari yangu kuacha nafasi ndani ya chama kwani ukiona viongozi wa juu  wanateuliwa  kuingia katika Serikali iliyopo madarakani  inayoongozwa na chama pinzani,  sisi wa ngazi za chini tutapata wapi sauti ya kushawishi wanachama wapya kujiunga na ACT-Wazalendo,” amesema.
Kiongozi huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kujiunga na chama chochote kwa sababu ni mapema mno na kwamba anataka akae pembeni na siasa kidogo aone nini cha kufanya kwanza. Bahati aliyasema hayo alipokuwa akijibu swali aliloulizwa, kama ana mpango wa kuhama chama hicho.
Uongozi wa chama hicho Mkoa wa Mbeya walisema kuwa wamesikia taarifa hizo lakini bado hawajapewa barua rasmi na kwamba wakishapewa watajua ni hatua gani za kuchukua.
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo,   Wilaya ya Mbeya, Ally Mbika alisema kujiengua kwa kada huyo ni pigo kwa chama kwani alikuwa ana mchango mkubwa wa ushawishi na kujenga umoja na mshikamano wa kweli wa ndani na nje ya mkoa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post