KWA MWENENDO HUU, SIMBA WASHINDWE WAO TU KUWANASA KAPOMBE, MANULA

Mambo yanayoendelea ndani ya Klabu ya Azam yameendelea kuteka vichwa vya habari ambapo sasa yameibuka mapya.
Wakati upepo ukiwa haujatulia taarifa za wachezaji Shomari Kapombe na Aishi Manula kuondoka klabuni hapo zimeshika kasi kutokana na mabadiliko ya kiuongozi ndani ya klabu hiyo.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimeeleza kuwa Bodi ya Azam imepitisha kuanzia msimu ujao mishahara ya wachezaji sasa itaanzia shilingi 600,000 huku kiasi cha juu kikieleza kuwa ni shilingi milioni 2 ambayo itakuwa ikitolewa kwa wachezaji wa kimataifa.
Ikiwa taarifa hizo zitakuwa na ukweli ni kuwa kutakuwa na uwezekano wa wachezaji wengi kuondoka hasa wale wenye majina makubwa kwa kuwa mfumo huo wa malipo unaweza kuwa kikwazo klabuni.
Manula na Kapombe wamekuwa wakitakiwa na klabu za Simba na Yanga wakati mikataba yao inaelekea kumalizika.
Mtu wa karibu wa ndani ya klabu hiyo amesema kuwa Kapombe kwa sasa analipa shilingi milioni 7 wakati Manula analipwa shilingi milioni 6, hivyo kiwango hicho cha mabadiliko kinaweza kuwaondoa au kuwapa urahisi klabu nyingine ziwasajiri kirahisi.
Kapombe alitua Azam FC msimu wa 2014 akitokea katika timu ya AS Cannes ya Ufaransa, ambayo nayo ilimchukua kutoka Simba kwa mkopo.
Kikosi cha kwanza cha Azam kwa sasa kipo kwenye mapumziko ya wiki tano baada ya kumalizika kwa msimu na kitarejea tena mazoezini Julai 3 mwaka huu, kuanza maandalizi ya msimu mpya.                        
Pia kuondoka kwa John Bocco, kumemfanya kocha huyo kupendekeza ongezeko la mshambuliaji mmoja mwenye uzoefu.
Ikumbukwe kuwa hadi sasa tayari Azam FC imepandisha wachezaji watano katika kikosi cha wakubwa kutoka kile cha vijana, wachezaji hao ni: Yahaya Zaidi, Stanley Stanslaus, Abbas Kapombe, Abdul Haji na Said Issa
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post