MADHARA YA KIAFYA YA KUVAA NGUO ZA KUBANA

SHARE:

Na Carolyne B Atangaza. Kwa msaada wa viguo vya kubana na vivazi vyote vinavyochonga shepu ya mwili, wengi mchana huonekana na maumbile...

Na Carolyne B Atangaza.
Kwa msaada wa viguo vya kubana na vivazi vyote vinavyochonga shepu ya mwili, wengi mchana huonekana na maumbile mazuri yanayovutia kuangalia na usiku wanarudi kwenye miili yao iliyotepweta baada ya kuzivua nguo zao.
Hatuoni tabu yoyote hata kujipaka mafuta ikibidi mradi tuweke kuingia kwenye jinzi za kubana au hata kuvaa ‘skini taiti’ mbili, vyovyote iwavyo ili mradi tuonekane wembamba kuliko tulivyo, tuonekane wazuri na wenye mvuto kuliko tulivyo na nyakati nyingine kwakuwa tunataka tuonekane vijana kuliko tulivyo.
Kama unaihusudu sana jinzi yako ya kubana, bila shaka ushawahi kupata tatizo la mwili kupatwa na ganzi kuanzia mapajani na kupoteza hisia kabisa kwenye mguu mzima mpaka chini. Madaktari wanaiita hali hii kwa jina la kitaalamu la meralgia paresthetica ambayo hutokea kwa sababu ya kukandamiza kwa muda mrefu mishipa ya neva za fahamu inayotoka kwenye kiunoni ambayo kazi yake ni kuleta hisia kwenye mapaja.
Mwili wa binadamu unatoa ishara fulani kama nguo au mapambo fulani tuliyovaa yanabana sana hata kama tukijidai kudharau tunayoyaona kwa macho yetu kupitia kioo ukiwa unajikagua kama umependeza ama la. Yafuatayo ni baadhi tu ya madhara ya kiafya unayoweza kuyapata kutokana na kuvaa nguo zinazobana mwili:
Ugumba
Dkt. George Bwesigye, daktari katika hospitali ya Najeera anatoa maelezo ambayo yanaweza kuwatisha wanaume wengi. “Kokwa zinazotengeneza mbegu za kiume zinatakiwa ziwe kwenye joto la chini tofauti na joto la mwili, ndio sababu zikawa nje ya mwili. Kwa hali hii, zinakuwa na uwezo wa kuzalisha mbegu za kiume kwa wingi. Kwahiyo, kuzibana na nguo kunazuia au kupunguza kwa kiasi kikubwa kazi yake hii ya msingi na huweza kusababisha ugumba.”
Maambukizi
Anasema kuwa chupi zinazobana husababisha joto linaloleta unyevu kwenye eneo hilo nyeti. Unyevu katika sehemu hiyo husababisha vjidudu vya fangasi kwa wanaume au utandu wa vijidudu unaosababisha muwasho na maambukizi kwa wanawake.
Mzunguko mdogo wa damu
Nguo za kubana zinazuia mzunguko unaotakiwa wa damu, ikizuia mzunguko wake wa kawaida wa kupeleka damu na kuirudisha kwenye moyo kwa ajili ya kutumika tena mwilini.
Hili linaleta maumivu, uvimbe au kuvimba/kupinda kwa mishipa ya damu ya miguu kutokana na presha kubwa inayopelekwa sehemu ya chini ya mwili. Kama una tatizo la kuwa na mafuta mengi mwilini, kuvaa nguo za kubana kunaliongeza tatizo hilo kwakuwa mzunguko wako wa damu utaathirika zaidi.
Matatizo ya mmeng’enyo wa chakula
Bwesigye anaendelea kueleza kuwa suruali na mikanda ambavyo vinabana sana tumbo vinakuwa vinalizuia tumbo kutanuka jambo ambalo ni la muhimu sana kwa ajili ya usagaji wa chakula ulichokula.
“Kwakuwa mfumo wa usagaji chakula haufanyi kazi sawa sawa, mtu atajikuta anapata viungulia na kujaa kwa kemikali tumboni, na matatizo mengine mengi,” amesema.
Maambukizo ya njia ya mkojo (UTI)
Mbunifu wa mavazi kwa watu mashuhuri, Solomon Tazibone amesema kuwa wanawake wanaovaa nguo za kubana mara nyingi sana hukwepa kutumia vyoo vya kadamnasi, ambavyo vinahatarisha wanawake wengi sana kupata maambukizi ya njia ya mkojo.
“Si rahisi kutua nguo zilizokubana sana hasa kwenye vyoo vinavyotumiwa na watu wengi. Kwahiyo wanawake wengi hujikuta wakizuia haja ndogo kwa saa kadhaa wakisubiri kwenda sehemu walizozizoea na salama kwao kama majumbani mwao,” anasema.
“Tatizo kubwa zaidi ni pale nguo hizi zinapovaliwa na mabinti wadogo. Tunaweza tukabisha lakini hali halisi ni kwamba wanaume wanapenda kuona vitu vinavyowavutia na hawatasita kumuita mtoto wa miaka 11 aliyevaa kaptura au hata kumuangalia kwa matamanio.
Kama wazazi ni jukumu lenu kuwalinda watoto wenu hata kama utaitwa mshamba au mkoloni.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MADHARA YA KIAFYA YA KUVAA NGUO ZA KUBANA
MADHARA YA KIAFYA YA KUVAA NGUO ZA KUBANA
https://2.bp.blogspot.com/-YJDEFHUdViI/WUZEthnq5fI/AAAAAAAAcXg/BgrnxXW7wlshpJ7_8TIsKQQbMQttq9mBgCLcBGAs/s1600/xIs-Wearing-Tight-Clothes-Bad-For-Your-Health-770x402-750x375.jpg.pagespeed.ic.6Efvpn7AZv.webp
https://2.bp.blogspot.com/-YJDEFHUdViI/WUZEthnq5fI/AAAAAAAAcXg/BgrnxXW7wlshpJ7_8TIsKQQbMQttq9mBgCLcBGAs/s72-c/xIs-Wearing-Tight-Clothes-Bad-For-Your-Health-770x402-750x375.jpg.pagespeed.ic.6Efvpn7AZv.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/06/madhara-ya-kiafya-ya-kuvaa-nguo-za.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/06/madhara-ya-kiafya-ya-kuvaa-nguo-za.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy