MAGUFULI AGOMA KUSOMESHA WATAKAOPATA MIMBA SHULENI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa hayupo tayari kusomesha watoto ambao watapata mimba wakiwa shuleni kuanzia shule za msingi mpaka sekondari.
Dkt. Magufuli amesema hayo leo akiwa Bagamoyo mkoani Pwani katika uzinduzi wa barabara ya Msata – Bagamoyo yenye urefu wa kilomita 64.
“Mimi ndani ya kipindi changu cha Urais hakuna mtoto mwenye mimba atakayerudi shule. Tunakuwa tunawafundisha kitu gani, kwamba unaweza kwenda kuzaa na ukarudi shule? Tukifanya hivyo hatuoni kwamba atakuja kuwafundisha wenzie wafanye kama alivyofanya yeye? Maana yake mchezo huo ni mtamu, na kila mmoja anapenda kuufanya,” amesema Rais Magufuli na kuongeza…
“Ukiwaruhusu wenye mimba warudi shuleni baada ya kuzaa, itafika mahali hata watoto wa darasa la kwanza watakuwa na watoto na mwisho watoto wa kike darasa zima watakuwa na watoto. Haya siyo maadili yetu. Tuwe na hofu ya Mungu. Hata kama ni mtoto wangu, aende akapate mimba aone kama nitamrudisha shule. Mtoto wa shule ya msingi hadi sekondari akipata mimba basi atafute kitu kingine cha kufanya, kwa sababu vya kufanya vipo vingi.”
“Wakati mwingine tukisikiliza hizi NGO (Taasisi Zisizo za Kiserikali) zitakuwa zinalipeleka Taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu hili halitatokea. NEVER. Na kama hizi NGO zinawapenda sana hao watoto, ni bora wao ndio wawafungulie shule zao maalumu za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.”
“Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata mbuzi na ng’ombe hawana. Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai.”
Rais Dkt. Magufuli amemsifu mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete kwa kulisimamia hili alipokuwa Bungeni mjini Dodoma kwakuwa tutakapoliruhusu ni sawa na kukiuka maadili ya Taifa letu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post