MAMA JANETH MAGUFULI ATOA MSAADA WA CHAKULA

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama Janeth Magufuli, leo ametembelea kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha New Life Orphanage kilichopo Boko jijini Dar es salaam kuwajulia hali pamoja na kutoa msaada wa vyakula kwa vituo nane. Chakula hicho kimetolewa kwa uongozi wa kituo cha New Life Orphanage kwa niaba ya vituo vingine.
Vituo vilivyonufaika na msaada huo ni New Life Orphanage (Boko), chenye watoto 121, Charambe Islamic, chenye watoto 54, Mwandaliwa Centre (Mbweni) chenye watoto 94, Al Madina Children Home (Tandale) chenye watoto 65, Ijangozaidia Orphanage Centre (Sinza) chenye watoto 1030, Azam Orphanage (Mbagala) chenye watoto 51, Hiari Orphanage (Chang’ombe) chenye watoto 41 na CHAKUWAMA (Sinza) chenye watoto 64.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post