MAMBO 6 WANANCHI WALIYOFURAHIA ZAIDI KATIKA BAJETI YA SERIKALI 2017/18

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango leo Juni 8, 2017 amewasilisha bungeni makadirio ya matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambapo imeungwa mkono na wabunge wengi huku wakisema kuwa itasaidia kuinua uchumi wa nchi.
Katika bajeti iliyowasilishwa leo, ni jumla ya Tsh trilioni 31.7 ambapo kati ya fedha hizo Tsh 19.9 ni fedha za ndani ambazo ni sawa na asilimia 63 ya fedha zote, huku fedha nyingine zikitarajiwa kutoka kwa washirika wa maendeleo pamoja na mikopo.
Katika bajeti hiyo, baadhi ya mambo yameshangiliwa sana na wabunge pamoja na wananchi kupitia mitandao ya kijamii. Hapa chini ni baadhi ya mambo hayo.
Serikali imepiga marufuku usafirishaji wa madini nje ya nchi yakitokea moja kwa moja kwenye migodi. Akisoma makadirio hayo ya mwaka wa fedha, Waziri Mpango alisema kuwa vitawekwa vituo maalum vyakuhakiki madini kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Hii itaisaidia serikali kupata thamani halisi ya madini hayo na kuweza kukusanya mapato stahiki.
Kingine kilichoshangiliwa sana ni kauli ya waziri wa fedha kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu kuwaonea walipakodi.
Akisoma bajeti hiyo, Waziri wa Fedha, Philip Mpango amwewaonya watumishi wa TRA kuacha mara moja tabia ya kuwabambikia kodi, kuwanyanayasa, au kuwakadiria kiwango cha juu walipakodi na mwisho wa siku wakashindwa kulipa kodi hiyo.
Jambo hili ambalo lilikuwa limepigiwa kelele sana na vyama vya upinzani leo limewafurahisha wengi kufuatia kauli hiyo ya serikali ambapo waziri mwenye dhamana alisema kuwa, mtumishi wa TRA atakayethibitika kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Hapa sasa serikali iliwagusa wamiliki wa magari ilipoamua kufuta ada ya mwaka ya magari (Annual Motor Vehicle Licence Fee) iliyokuwa ikilipwa na kila mmiliki wa gari kwa mwaka. Ada hii ilitakiwa kulipwa bila kujali kama gari linafanya kazi au limeegeshwa sababu ni libovu.
Serikali imetangaza kufuta ada hiyo ambapo sasa italipwa mara moja tu pale gari litakapokuwa likisajiliwa na baada ya hapo italipwa kupitia kwenye mafuta ambapo kama gari halitotumika inamaana hautalipia kwa sababu hautaliwekea mafuta, tofauti na ilivyokuwa awali.
Aidha, jambo lingine lililoungwa mkono na kufurahiwa na wengi ni uamuzi wa serikali kufuta kodi ya usafirishaji (Transit) kwa magari yaliyokuwa yakisafirisha mizigo kwenda maeneo mbalimbali nchi na nje ya nchi.
Baadhi ya waliopata nafasi ya kutolea maoni jambo hili wamesema kuwa, kwa sasa serikali itaweza kuvutia wafanyabiashara wengi kutumia bandari zetu kutokana na kuondolewa kwa kodi hiyo ambayo ilikuwa ikilalamikiwa sana na wafanyabiashara na hata kupelekea baadhi ya kusitisha kupitisha mizigo yao kwenda bandari ya Dar es Salaam.
Seikali imetangaza kufuta ushuru wa mazao kwa wakulima ambao watakuwa wakisafirisha kutoka halmashauri moja kwenda nyingine kama mazao yao yatakuwa na uzito chini ya tani moja.
Aidha, katika ushuru wa asilimia 5 uliokuwa ukitozwa na halamshauri katika msoko mbalimbali nchini, serikali impenguza hadi asilimia 3 kwa mazao ya biashara na asilimia 2 kwa mazao ya chakula.
Katika kuhakikisha inavutia wawekezaji nchini, serikali imesamehe kodi ya ongezeko la dhamani (VAT) kwenye bidhaa za mtaji ili kupunguza gharama za kuagiza mashine na kuvutia uwekezaji sekta ya viwanda.
Katika msamaha huo, endapo mwekezaji kutoka nje wa ndani ya nchi ataagiza mashine kwa ajili ya kufungua kiwanda, hatolipia VAT ikiwa ni mkakati wa serikali kuvutia wawekezaji na kuifikia Tanzania ya viwanda.
Baada ya waziri mwenye dhamana kuwasilisha bajeti hiyo, wabunge wanatarajiw akuanza mjadala Juni 12 mwaka huu kuhus mapendekezo au maboresho waliyonayo katika bajeti hiyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post