MAMBO YANAYOOGOPWA ZAIDI NA WANAWAKE TANZANIA

SHARE:

Na Devotha John Woga ni hali unayoipata ukiwa na wasiwasi au hofu kwamba jambo fulani baya litatokea. Kama binadamu mwengine yeyote, ...

Na Devotha John
Woga ni hali unayoipata ukiwa na wasiwasi au hofu kwamba jambo fulani baya litatokea. Kama binadamu mwengine yeyote, wanawake wanajikuta  mara kwa mara wakihofia mpaka inaathiri shughuli zao au uwezo wao wa kufanya maamuzi juu ya jambo fulani.
Kwa sababu ya hofu hii, wengi wanapoteza uwezo wao wa kujiamini, kuyumba kwenye mahusiano yao na mara nyingine hofu inasababisha wengine kujiua.
Kuwa kwenye ndoa inamaanisha umekubali kuishi na mtu mwengine kwa maisha yako yote yaliyobaki, lakini mtu akitawaliwa na woga, utampelekea mara zote kuwa na wasiwasi wa labda ndoa hiyo itapoteza mvuto na watakuja kuachana na mumewe.
Kuna woga ambao huwapata wanawake wengi walio kwenye ndoa na ambao hawamo kwenye ndoa pia ambao kiujumla unaweza kuathiri maisha yao. Zifuatazo ni aina nane za woga unaowakumba wanawake wengi hapa Tanzania.
Woga wa kufa
Pamela Israel (35) ambaye ni mama wa watoto watatu anakiri kuwa akiwaza kufa anapata woga, hasa akiwaza kuwaacha watoto wake anaowapenda kutavyowaletea huzuni na maumivu.
“Haimaanishi kwamba mume wangu hatawapa malezi mazuri lakini wasiwasi wangu ni kuwaacha wakiwa na umri mdogo sana. Naomba Mungu anijalie umri mrefu niwalee wanangu mpaka nao waanzishe familia zao,” amesema Pamela na kuongeza “..mbali na hilo, watoto wakiwa wadogo wanahitaji malezi na kuwa karibu na mama yao.”
Pamela anasema kwamba woga huu unamfanya kuongeza maombi ili aweze kuja kuwaona wajukuu zake. Mara nyingi anakuwa na wasiwasi kwamba atakapokufa, mume wake ataoa mwanamke mwingine ambaye bila shaka hatawapenda watoto wake kama anavyowapenda yeye. Pia anaogopa endapo mumewe au mwanaye atakapofariki, jambo linalowaogopesha karibu wanawake wote na kuwakosesha usingizi.
Woga wa ukewenza
Bestina Lwiva (32) anasema kuwa dini yake inaruhusu mume kuwa na mke zaidi ya mmoja na kwamba mawazo tu ya kwamba mumewe kuongoza mke mwengine huwa yanamnyong’onyesha.
Sheila Abdul (38) pia anahofia kuwa ipo siku mumewe anaweza kuongeza mwanamke mwingine kwakuwa dini inaruhusu hilo.
“Nipo kwenye ndoa kwa miaka kumi sasa. Sijawahi kutilia shaka uaminifu wa mume wangu kwangu na sijawahi hata kumuwazia kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa. Jambo pekee ambalo sitaki hata kumliwaza ni siku atakayokuja kuniomba ruhusa ya kuoa mke mwengine,” anasema.
Anaongeza kusema kuwa kama mwanaue anaoa mwanamke mwingine, ni wazi kuwa mambo hayawezi kuwa sawa na yalivyokuwa awali tena.
“Najua kwamba dini inatufundisha wanawake wana haki sawa, lakini sipendi awe na mwanamke mwingine kwa kisingizio cha dini,” ameongeza.
Woga wa talaka
Tunaelewa kwamba ndoa ni ahadi kuu kwa wapenzi kwa lengo la kuishi pamoja kwa maisha yao yote yaliyobaki, lakini baadhi ya wanawake wanahofia kwamba muunganiko huo utakuja kuvunjika siku moja na kuwaacha wakiwa kwenye majonzi na aibu.
Safina Mziray (25) ameolewa hivi karibuni lakini tayari ameingiwa na hofu hii kwakuwa hajui kama ndoa yake itadumu. Anasema kwamba lolote linaweza kutokea na kusababisha aachike.
“Najua tunapendana sana lakini lolote linaweza kutokea na kuingilia mipango mizuri tuliyojiwekea kimaisha,” anasema.
Woga wa kuwaacha watoto na mfanyakazi
Bila shaka wanawake wanahofia usalama wa mtoto wake mchanga anapobaki na msaidizi wa kazi za nyumbani baada ya kuisha kwa likizo ya uzazi. Wengi wanafikiria kuwa watoto wao watateswa na wafanyakazi hawa, pia wanaamini hakuna anayeweza kumjali mwanae kwa upendo zaidi yake.
“Huu ndio muda ninaokuwa na wasiwasi kupita kiasi. Nikiwa naangalia video za baadhi ya wafanyakazi wa ndani wanavyowatesa watoto, naanza kufikiria na wa kwangu atakuwa anafanyiwa hivi hivi,” anasema Diana (30) mama wa watoto wawili.
Woga wa mume kutokuwa muaminifu
Wapenzi mara zote wanaogopa wenza wao kutokuwa waaminifu. Wanasema kuwa mnaweza kufunga ndoa takatifu Kanisani na kwa sherehe kubwa sana na bado mkaendeleza mahusiano ya nje ya ndoa, jambo linaloleta migogoro isiyoisha.
Wanawake mara zote wanapenda kuwa kwenye mahusiano yanayodumu muda mrefu, lakini kama mambo yakibadilika , mara zote wanajikuta wanalazimika kuvumilia maumivu makali sana.
Fatuma Ramadhan (27) anasema kuwa tangu aachane na mpenzi wake, amekuwa anaishi kwa woga sana. Mpenzi wake huyo kisirisiri alioa mwanamke mwengine, na toka hapo imani yake kwa wanaume imepotea kabisa na hawezi kuanzishwa mahusiano mengine.
“Nilipokuja kugundua kuwa mpenzi wangu alikuwa na mwanamke mwengine niliumia sana na nilikuwa na wasiwasi muda wote. Ilikuwa ngumu sana kulivumilia,” amesema na kuongeza kuwa “…tangu muda huo siamini mwanaume yeyote yule. Najua kwamba wanaume wote wanafanana tabia na nimeamua kuwa peke yangu.”
Woga wa kutopata mume maisha yote
Monica Michael (30) ni mhasibu. Anasema kuwa ana kila kitu anachohitaji maishani mwake lakini anachohitaji kwa sasa ni mpenzi wa kudumu kwakuwa ana wasiwasi wa kubaki mwenyewe maisha yake yote.
Ana elimu nzuri kiwango cha shahada ya chuo kikuu, na sasa anamiliki nyumba na gari. Kiungo pekee kinachokosekana kukamilisha maisha mwanaume wa kumpenda.
“Mara nyingine huwa nafikiria nianzishe mahusiano na mwanaume yeyote tu, tuanzishe familia ili na mimi nionekane nimekamilika. Pia itafanya watu wangu wa karibu waniheshimu,” amesema na kuongeza kuwa kibaiolojia anaona amechelewa sana.
Kuna baadhi ya wanawake huwa hawaridhiki na mafanikio walivyofikia. Wataalamu wanasema kuwa kwa hali kama hiyo, wengine wanahitaji kujituliza na kuwa na mtazamo chanya wa kimaisha ya kwamba mambo yatanyooka bila kujali mahusiano yako ya kimapenzi au ya kazini.
Woga wa kutokuwa na uwezo wa kubeba mimba
Malpa Kimaro (30) anasema kuwa anaogopa sana kwamba labda hataweza kuja kubeba mimba maisha yake yote baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na tatizo hilo.
“Tumeoana kwa miaka minne sasa, tumefanya vipimo vingi ambavyo ni vya gharama kubwa sana lakini mpaka sasa hatujafanikiwa kupata mtoto,” anasema.
“Hiki ndio kitu ninachoogopa zaidi. Nina wasiwasi labda sitakuja kuwa na watoto wangu mwenyewe maishani mwangu. Huwa najiona mpweke sana nikiona wanawake wenzangu wakiwa wamewabeba au kuwashika mikono watoto wao na bado naamini kuwa Mungu hakuniumba mgumba,” amesema.
Woga wa kukataliwa
Sote tumeumbwa ili kujenga mahusiano, kwa namna moja ama nyingine, lakini mara nyingine haiwi rahisi kiasi hicho kujenga mahusiano haya. Tunaweza kutaka kuwa miongoni mwa kundi fulani au darasa au kuwa pamoja na watu fulani.
Kwahiyo tunapowekwa kando kwenye mahusiano au makundi hayo tunapata hisia za kukataliwa, kutengwa au hata kudharaulika. Kwa Maria Michael (25), woga wake mkuu uliongezeka baada ya kukataliwa na mwanaume aliyekuwa anampenda sana ambaye alitamani awe mpenzi wake. Anasema kuwa alipokuwa chuo kikuu, alimpenda kijana mmoja lakini alishindwa kumueleza hisia zake.
“Tulikuwa tupo darasa moja na tulikuwa katika kundi moja la kujisomea, lakini alinikataa kwakuwa hakuwa ananipenda,” alisema.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAMBO YANAYOOGOPWA ZAIDI NA WANAWAKE TANZANIA
MAMBO YANAYOOGOPWA ZAIDI NA WANAWAKE TANZANIA
https://3.bp.blogspot.com/-tnCQT6LF0WY/WUfGFgm91TI/AAAAAAAAcZg/9gRtwqEb0dcWbTOOI9SOMSlRqAZVdrQPACLcBGAs/s1600/o-BLACK-WOMAN-SCARED-facebook-750x375.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-tnCQT6LF0WY/WUfGFgm91TI/AAAAAAAAcZg/9gRtwqEb0dcWbTOOI9SOMSlRqAZVdrQPACLcBGAs/s72-c/o-BLACK-WOMAN-SCARED-facebook-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/06/mambo-yanayoogopwa-zaidi-na-wanawake.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/06/mambo-yanayoogopwa-zaidi-na-wanawake.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy