MATUMAINI AFUNGUKA UKIMYA WAKE NA ANGUKO LA FILAMU NCHINI

Msanii wa filamu za vichekesho nchini Tanzania Matumaini aliyetamba kwa filamu ya Nyama choma, Mganga Nyambu na Ndoa ya Kinyambi na matumaini  amefunguka leo kuhusu ukimya wake katika tasnia ya filamu nchini.
Akiongea na mtandao huu,Matumaini amesema soko la filamu limekuwa gumu  limesababisha wasanii na waandaaji wengi kukaa kimya.
“Tunaandaa filamu lakini soko linatufanya tusiziingize maana hakuna wasambazaji wanaopokea kazi kwa  kupata hasara ndiyo maana tumeamua kukaa kimya “alisema Matumaini.
Hali ya soko la filamu limekuwa gumu kutokana na watanzania wengi kujikita katika kufatilia tamthilia na filamu za nje na kuacha kuwasapoti wazawa ili kukuza na kuinua uchumi wa waigizaji na Taifa kwa ujumla.
Matumaini amesema hana budi kutumia fursa hii kuwaomba mashabiki na watannzania kwa ujumla kuwa wazalendo kwa kununua kazi za wazawa ili waweze kufanya kazi nzuri  na zenye ubora.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post