MAZUNGUMZO YA MBOWE NA WEMA, STEVE NYERERE AFUNGUKA

Siku mbili zilizopita kipande cha rekodi ya mazungumzo yanayodhaniwa kuwa ni kati ya Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Aikael Mbowe akiwa anamtongoza mwanadada Wema Sepetu kilisambazwa kwa kasi sana katika mitandandao ya kijamii nchini.
Related image
Mwanadada Wema Sepetu begani kwa Freeman Mbowe
Baada ya kusambaa kwa rekodi hiyo kumekuwa na tetesi nyingi zikijaribu kusema wahusika halisi wa sauti hizo ni nani ambapo jina la Steve Nyerere limekuwa likitajwa kuhusika kwa kiasi kikubwa. Steve ametajwa sana labda kwakuwa anatambulika kuwa na kipaji na uwezo mkubwa wa kuigiza kwa usahihi wa hali ya juu sauti za watu mbalimbali wenye majina au hadhi ya juu nchini.
Baada ya shutuma hizi, Steve ameona ni bora atoe tamko akielezea upande wake wa habari hizo akikanusa uhusika wake kwa kusema kuwa hana sababu, ugomvi wala hana uwezo wa kuongea Kingereza kilichoongewa na Bwana “Mbowe” aliyesikika katika kipande hicho.
“Kwanza mimi toka nimeanza kuigiza sauti sijawahi kuigiza sauti za viongozi wa chama fulani. Pili, kutongoza napo sio dhambi, ni sunna (akimaanisha ni jambo jema tu kwa mwanaume yoyote kulifanya). Tatu, sio kila kitu ambacho kimefanywa na familia fulani basi Steve anahusika. Limenikera na kuniumiza sana. Pia sio kwa Kingereza kile cha kubembeleza vile, nina uwezo huo? Na pia sio mimi peke yangu ninayeweza kuigiza sauti za watu, waigizaji wapo wengi.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post