MBEYA: BABA ATOA USHAHIDI ULIOSAIDIA MWANAE AHUKUMIWE KUNYONGWA

Geoffrey Sichizya (27) amehukumiwa kunyongwa hadi kufa jana baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ikisaidiwa na ushahidi wa baba mzazi wa mshtakiwa kumtia hatiani kwa kosa la kumuua kwa kukusudia babu yake (Labson Sichizya) ili achukue ng’ombe wake tisa.
Akisoma hukumu hiyo kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana, Jaji wa Mahakama Kuu, Atuganile Ngwala alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na Meas Sichizya (baba mzazi wa mshtakiwa), pamoja na Mashaka Sichizya (ndugu), ambao walimkamata mshtakiwa siku ya tukio wakiwa na viongozi wa kijiji na kumpeleka polisi.
Awali, ilidaiwa Mahakamani hapo na wakili wa Serikali Ofmedy Mtenga kwamba mshtakiwa alimkaba koo babu yake hadi kufa Novemba 19, 2012 saa 2:00 asubuhi katika kijiji cha Sakamwela, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.
Mshtakiwa huyo baada ya kumuua babu yake kwa kumkaba koo, alimfunga na kamba ya chandarua shingoni na kumning’iniza kwenye mti nyuma ya nyumba yake ili ionekane kama marehemu alijinyonga.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post