MBUNGE LUCY OWENYA ALIVYOPOKEA TAARIFA ZA KIFO CHA BABA YAKE MZEE NDESAMBURO AKIWA BUNGENI

Tanzania leo imekumbwa na simanzi kubwa kufuatia kifo cha mwanasiasa mkongwe na Mbunge Mstaafu wa Moshi Mjini (CHADEMA), Philemon Ndesamburo aliyefariki mapema leo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.
Miongoni mwa watu wengi waliopokea taarifa hizi kwa huzuni kubwa ni mtoto wa Mzee Ndesamburo ambaye naye ni Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Lucy Owenya.
Taarifa za kifo cha Mzee Ndesamburio zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii majira ya asubuhi ambapo Mbunge huyo alikuwa bungeni akisubiri zamu yake ya kuchangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ambapo Bunge leo lilikuwa likiongozwa na Mwenyekiti, Andrew Chenge.
Wakati Chenge akingoza Bunge ilipofika wakati wa Lucy Owenya kuchangia alimruka kwa makusudi sababu ya taarifa za kifo cha baba yake, lakini kwavile mbunge huyo hakuwa na taarifa hizo, alisimama na kumwambia Mwenyekiti kuwa ilikuwa zamu yake kuchangia, hivyo akaruhusiwa kuchangia.
“Niliamua kumruhusu baada ya yeye kuweka msisitizo sana, lakini hakuwa akijua kuhusu taarifa za kifo cha baba yake ambaye alikuwa mbunge mwenzetu kwenye Bunge la 2015” alisema Chenge.
Baada ya kumaliza kutoa mchango wake, Mbunge mwenzake, Suzan Lyimo (CHADEMA) alimuita nje, lakini alionekana kutokujua chochote kuhusu baba yake kufariki sababu hakuwa amepitia simu yake.
Mbunge wa Viti Maalum-CHADEMA, Lucy Owenya akilia kwa uchungu baada ya kupata taarifa za kifo cha baba yake, Mbunge Mstaafu Mzee Ndesamburo.
Wakati huo akitoka, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe naye alikuwa nje tayari akimsubiria katika mlango wabunge. Na muda mfupi baadae wabunge wa upinzani walitoka nje kumfariji mwenzao huyo.

Mbunge huyo alielekea anapoishi mjini Dodoma baada ya kupewa taarifa hizo na kikao cha bunge kilipoahirishwa, wabunge wengi walikwenda kumfariji Lucy, ambaye alikuwa akilia kwa uchungu sana.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post