MBUNGE PHILEMON NDESAMBURO ALIJITABIRIA KIFO CHAKE?

Mwanansiasa mkongwe na Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburi unaweza kusema kuwa alijitabiria kifo chake kwani siku chache kabla ya kifo chake aliwaita watoto wake wote 11 na kuwasaa waishi kwa upendo na amani siku zote.
Hayo yalibainishwa jana na mtoto wa mzee huyo, Sindato Ndesamburo alipokuwa akiongea nyumbani kwa baba yake KDC, Barabara ya Mbokomu, Kiboroloni Manispaa ya Moshi Mjini, Mkoa wa Kilimanjaro.
Mtoto huyo alisema kuwa baba yao alikuwa akikutana nao katika vikao vya familia, au kipindi cha sikukuu na kuwapa mawaidha, lakini kipindi hiki kilikuwa tofauti kwani kulikuwa hamna kikao cha familia au sikukuu lakini aliwaita na kuwaasa, isitokee hata siku moja wakafarakana.
Kuhusu maziko ya kiongozi huyo yatafanyika siku ya Jumanne nyumbani kwake lakini kabla ya hapo siku ya Jumatatu ataagwa katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post