MENEJA WA MGODI WA ACACIA AKAMATWA

Meneja Ardhi wa Mgodi wa Acacia North Mara, Peter Enger alikamatwa juzi wa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime kufuatia kampuni hiyo kushindwa kuwalipa wananchi fidia kwa miaka mitatu.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga alisema kuwa alifikia uamuzi wa kutaka meneja huyo akatwe ikiwa ni suluhisho la  fidia ya wananchi.
Zaidi ya wakazi 1,000 kutoka katika vitongoji Nyamichele, Muryambai  na vijiji vya Kewanja, Matongo, Kerende, Nyakunguru, na nyamwaga wanadai fidia za mali zao yakiwamo mazao na nyuma ambapo juzi waliandamana mpaka kwenye mgodi huo wakishinikiza kusikilizwa kwa malalamiko yao.
Luoga alisema kuwa aliagiza meneja huyo akamatwe na kupelekwa Kituo cha Polisi Musoma baada ya kufika mgodini hapo kutuliza ghasia hizo.
Awali malipo ya fidia za wananchi yalichelewa kwa kudaiwa kuwapo majina hewa ya wananchi ambapo serikali iliingilia kati lakini bado hadi leo hawajalipwa. Mkuu huyo wa Wilaya  aliuagiza uongozi wa mgodi kuwalipa fidia wale wote ambao majina yao hayana utata.
Wananchi hao walisema mbele ya kiongozi wa wilaya kuwa mgodi huo umewafanya washindwe kulima mashamba yao yaliyochukuliwa na kufanyiwa tathmini kwa ajili ya malipo tangu miaka mitatu iliyopita.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post