MEYA NA MKUU WA MKOA WA ARUSHA ‘WATIFUANA’ TENA

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Kalisti Lazaro Bukhay ametoa siku saba kwa Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo kumwomba radhi kwa kumuweka ndani bila kosa wakati walipokwenda katika Shule ya Msingi la Lucky Vicent kukabidhi rambirambi kwa wazazi waliofiwa na watoto wao katika ajali ya basi la shule hiyo.
Meya ametaka RC Gambo kumuomba radhi yeye pamoja na viongozi wa dini, madiwani na wawakilishi waliokuwa wameandamana pamoja siku hiyo Mei 18 mwaka huu na kukamatwa kwa agizo la kiongozi huyo bila kuambiwa kosa lao ni lipi.
Kalist Lazaro aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa, kitendo cha yeye kukamatwa pamoja na viongozi wa dini kilikuwa ni kinyume na sheria kwa sababu wakamataji hawakuwa na kibali cha mahakama cha kufanya hivyo, na pia hawakueleza kosa lao, kitu ambacho alikiita ni matumizi mabaya ya madaraka.
Aidha, Meya alisema jambo ambalo alilishangaa kutoka kwa kiongozi huyo ni kuamuru kuwekwa ndani Paroko na kiongozi wa dini ya Kiislamu. Meya alimtaka RC Gambo ajitafakari kama bado anafaa kuongoza mkoa huo kwa sababu inaonekana anadai kuwatumikia wananchi lakini hawaheshimu.
Hadi sasa Mkuu wa Mkoa wa Arusha hajazungumzia kauli hiyo ya Meya wa Jiji ya kumtaka kuwaomba msahama kwa kuamuru wawekwe ndani.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post