MILIONI 50 KILA KIJJI KUANZA JULAI MOSI

Serikali imetangaza kuwa ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji nchini itaanza kutekeleza wakati wowote baada ya kupitishwa kwa bajeti ya fedha ya mwaka 2017/2018.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji alitoa maelezo hayo Bungeni wakati akifanya majumuisho ya wizara yake na kusema kwamba kiasi cha shilingi bilioni 60 kimetengwa kwa ajili ya kutekeleza ahadi hiyo ya Rais.
Alisema kuwa ahadi hiyo iliyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwenye kampuni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 itatekelezwa mwaka ujao wa fedha.
“Tunaangalia utawala wa fedha hizi, tunaangalia pia namna gani nzuri ya kuzisambaza ili tukianza tusifanye kazi kwa kubatisha bahatisha maana huko nyuma yaliwahi kufanyika makossa, sasa wakati huu lazima tuwe makini na hatutaki kurudia makossa,” alisema Dkt. Kijaji.
Amesema kuwa Serikali inataka kuhakikisha kunakuwa na mfumo mzuri wa ugawaji wa fedha hizo ili ziweze kuleta matokeo chanya kwa watakaopewa na kuwatahadharisha wananchi kuwa fedha hizo ni mkopo na si ruzuku.
“Hatutaki fedha hizi zipotee maana hii si ruzuku na wananchi lazima watambue hivi. Tunataka fedha ziwafikie watu wanaohusika, tunataka tujue nani anataka kiasi gani na anataka kufanya nini na fedha jizi ili tuwe na uhakika wa wahusika kuzirejesha, na je, ni mfumo gani utatumika wakati wa kuzirejesha,” alisema Dkt. Kijaji.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post