MSANII ALIYESHIKA KICHWA BANDIA CHA TRUMP KILICHOKATWA KUSHTAKIWA

Msanii mchekeshaji raia wa Marekani mwanamama, Cathy Griffin aliyeonekana ‘live’ kupitia kipindi cha TV kinachorushwa na CNN akiwa ameshika kinyago kinachofanana kabisa na kichwa cha Rais Trump huenda akashtakiwa kutokana na kile kilichotajwa kama kuvuka mipaka ya Uhuru wa habari.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 57 alionekana akiwa amebeba kinyago cha Rais Trump akiwa amekatwa kichwa, jambo ambalo limezua hasira miongoni mwa watu wengi wakiwemo wapinzani wa Trump nchini marekani.
Baada ya Tukio hilo Kituo cha TV cha CNN kilitangaza kumfukuza kazi msanii huyo na kukifuta kipindi chake mara moja
Baadhi ya watu maarufu nchini Marekani akiwemo Rais Trump mwenyewe wamekilaani kitendo hicho na kusema ni dhihaka na udhalilishaji kwa familia za Wanajeshi na baadhi ya Waandishi wa Habari wa Marekani waliochinjwa na Kikundi cha kigaidi cha ISIS.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Ulinzi wa Rais nchini marekani (Secret Service) imesema uchunguzi umekamilika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani Cathy Griffin.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post