MSIKILIZE MTEJA AKITISHIA KUISHTAKI TIGO SABABU YA OFA YA JAZA UJAZWE

Mmoja wa wateja wa Tigo aliyejitambulisha kwa jina la Joseph kutokea mkoani Morogoro ametishia kuipelekea Kampuni hiyo ya Mawasiliano mahakamani kwa madai kuwa ofa ya Jaza Ujazwe, kwake yeye inakiuka maadili ya jamii yake.
Joseph anasikika kwenye simu akiwa amepiga simu kupitia namba ya huduma kwa wateja na kusema kuwa amekuwa mteja wa kampuni hiyo kwa muda mrefu sasa lakini hataki jummbe za ofa hiyo ya Jaza Ujazwe ambazo amekua akitumiwa.
Aidha, Joseph amewashangaa Tigo kwa kuleta majina ya ofa ambayo yana utata huku akiwaambia kuwa Tanzania kuna makabila tofauti tofauti na kuwa neno moja kwenye jamii moja linaweza kuwa sawa, ila kwa wengine lisiwe hivyo.
Mteja huyo alisema kuwa kwake yeye neno hilo ni tusi na kama wataendelea kumtumia jumbe zenye maneno hayo atawashtaki. Msikilize hapa chini;JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post