MTOTO WA ALIYEKUWA RAIS WA ZANZIBAR AJIUNGA CUF, ASEMA ANA MENGI MOYONI

Mtoto wa wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume juzi alitangaza rasmi kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF) ambapo alipokelewa na kupewa kadi ya uanachama na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.
Halfa ya kukabidhiwa kadi ya chama ilifanyikia nyumbani kwa Maalim Seif Chukwani Zanzibar ambapo ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Ahmed Mazrui.
Ikiwa sasa ni takribani siku tatu zimepita tangu Akhsa Abeid Aman Karume alipojiunga rasmi na chama hicho kikuu cha upinzani Zanzibar, amesema kuwa anayomengi ya kuzungumza lakini anasubiri kwanza mwezi mtukufu upite.
Wakati Akhsa akiyasema hayo, uongozi wa CUF visiwani humo umesema kuwa kuna viongozi wengine 12 kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) watakaojiunga CUF karibuni.
Akizungumzia suala la mtoto wa Rais Karume kujiunga CUF, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Salim Bimani amesema kuwa inaonyesha namna chama hicho kinavyokubalika Zanzibar na kwa watanzania wote. Alisema kuwa wananchama wengi wa CCM bado wanachuki na chama hicho kufuatia kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa 2015 na kadiri siku zinavyokwenda watazidi kuhama.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post