NAHODHA WA EVERTON ALIYELETWA NA SPORTPESA AJICHANGANYA NA VIJANA WA BONGO

Leon Osman huyu ni nahodha wa zamani wa Everton, yuko jijini Dar es Salaam katika ziara fupi iliyoratibiwa na Kampuni ya SportPesa.
Leon ameongoza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Everton, Robert Elstone ambaye kitaaluma ni mhasibu.

Wawili hao wakiwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam walipata nafasi ya kuona baadhi ya wachezaji wenye vipaji ambao walipata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwa muda mfupi.

Nahodha huyo pia alipata nafasi ya kupiga danadana kwa muda mfupi na wachezaji hao wa Tanzania ambao ni taifa la baadaye.

Kati ya watu waliokuwepo uwanjani ni mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe. Pia Ofisa Mtendaji Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov.

Osman aliichezea Everton katika maisha yake yote ya soka kuanzia mwaka 2000 hadi 2016 japokuwa hapo kati wakati anaanza kukomaa alitolewa kwa mkopo kwenda Carlisle United na Derby County.

Kwa sasa umri wake ni miaka 36
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post