PICHA 10: MAKAMU WA RAIS AONGOZA WANANCHI KATIKA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan jana ameongoza mamia ya wananchi waliojitokea katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
Makamu wa Rais katika maadhimisho hayo amepata wasaa wa kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara lakini pia kushiriki katika kongamano lililoandaliwa kwa lengo la kujadili athari za uharibifu wa mazingira na namna bora ya kukabiliana nazo.
Maadhimisho ya kilele cha siku ya mazingira duniani kitaifa yamefanyika Butiama mkoani Mara lengo kubwa likiwa ni kutambua na kuuenzi kwa vitendo mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika kulinda, kutunza na kuhifadhi mazingira.
Mbali na Makamu wa Rais, wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kaburi, Mke wa Mwl. Nyerere, Mama Maria Nyerere viongozi mbalimbali wa serikali, wanaharakati wa kutunza mazingira na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post