PICHA: BEN POL AMKUNA EBITOKE, WAKUTANA NA KUYAJENGA

Baada ya mwanadada kwenye tasnia ya uchekeshaji Ebitoke kufunguka ya kwamba mwanaume anayemzimia sana ni miondoko ya RnB nchini, Bernard Paul almaarufu Ben Pol, watu wengi hasa kupitia mitandao ya kijamii walijitokeza kutoa maoni yao kuhusu kauli ya mwanadada huyo.
Wengi walimponda sana kwa kumwambia aache kujipendekeza au kwamba anatafuta kiki ajulikane na mwanamuziki huyo na wale ma-opportunist a.k.a wazee wa ganda la ndizi kuteleza wakaamua hata kufungua akaunti za instagram kujaribu kupata followers wengi kupitia kastori hako.
Pamoja na maneno lukuki toka kwa mashabiki na mabingwa wa chuki binafsi (haters) wawili hao wamekutana na kula bata kiaina kisha kupiga photo shoot. Picha hizo zimelipua upya wafatiliaji wa mitandao ya kijamii hasa baada ya kila mmoja kuweka kwenye akaunti yake na kuandika ya moyoni mwake.
Tazama picha zifuatazo na kilichoandikwa na kila mmoja kumuelezea mwenzie:
Katika ukurasa wake wa Instagram, mwanamuzikiBen Pol ameandika:
“Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba kwa Mhusika? Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao, Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu duniani sisi sote TUNAPITA, na labda huyo Mtu kesho hatokuwepo. Ebitoke umenifundisha jambo KUBWA SANA maishani, najua wengi walikubeza sana , wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na Mimi.. lakini huwezi amini Mimi nimefurahi mno!! kukutana na wewe na kuongea, na nimepata jambo kubwa sana. Na Nitayaishi Maneno yako ๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ˜. Nakushukuru sana, Mwenyezi Mungu akuzidishie. You are THE BEST ๐Ÿ’ช๐Ÿพ!!@ebitoke #blessed๐Ÿ™๐Ÿฝ
Mwanadada Ebitoke safari hii amekuwa na machache kuelezea hisia zake kwa kuandika:
Asante Mungu
๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜ You are the real GENTLEMAN
@iambenpol ๐Ÿ’‘ ”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post