PICHA: KARDINALI PENGO AREJEA NCHINI AKITOKEA KUTIBIWA MAREKANI

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyekuwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu amerejea nchini jana.
Kardinali Pengo alirejea jana akitokea Dubai ambapo alipumzika kwa siku moja kutoka New York kufuatia ushauri wa madaktari waliokuwa wakimtibu.
Taarifa za kurejea kwa kiongozi huyo zilitolewa na Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa ambapo alindika kupitia ukurasa wake wa Facebook na kumkaribisha kiongozi huyo.
Kardinali Pengo alikwenda nchini Marekani mapema Mei 2 mwaka huu ambapo ilielezwa amekwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya pamoja na matibabu lakini haikuwekwa wazi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa gani.
Akiwa Dubai, Pengo alipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu Dk Jakaya Kikwete aliyekuwa njiani akielekea nchini Canada. Rais Kikwete aliandikwa ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Twitter akisema amefurahi kumuona Pengo akiwa na afya njema.
View image on TwitterView image on Twitter
Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.
Askofu Nzigilwa alisema kuwa, Kardinali Pengo anawashukuru waamini na watu wote wenye mapenzi mema waliokuwa wakimuombea na kumtakia matashi mema wakati wote alipokuwa kwenye matibabu.

 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post