PICHA YA MTOTO WA CHEICK TIOTE AKIMLILIA BABA YAKE YAWAGUSA WENGI

Kifo cha kiungo wa zamani wa Newcastle United, Cheick Tiote bado ni gumzo duniani kutokana na mchezaji huyo kufariki akiwa uwanjani akifanya mazoezi ya soka, lakini sasa picha ya mtoto wa kiungo wa Tiote imewasikitisha na kuwagusa wengi kutokana na ujumbe wake.
Picha ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka 3 anayejulikana kwa jina la Rafael, akiwa amevaa jezi ya Newcastle United imesambaa mitandaoni ikimuonyesha upande wa nyuma ambapo ina ujumbe ulioandikwa:  ‘R.I.P Daddy 24.’

Namba 24 imewakilisha namba ya jezi ambayo alikuwa akiivaa staa huyo alipokuwa Newcastle kwa miaka kadhaa.

Mashabiki wengi wa soka wametoa maoni yao kuonekana kuguswa na picha hiyo na kusema inasikitisha.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post