PRESHA IMEONGEZEKA, ANTOINE GRIEZMANN AOMBA KUONDOKA ATLETICO MADRID

Straika Antoine Griezmann ameiambia klabu yake ya Atletico Madrid kuwa anataka kuondoka klabuni hapo.
Hizo ni taarifa kutoka Hispania ambazo zimeibuka wakati ambapo mchezaji huyo yupo katika presha kubwa ya kuwaniwa na Manchester United chini ya Kocha Jose Mourinho.
Siku kadhaa zilizopita Mourinho aliulizwa juu ya suala hilo la kumsajili Mfaransa huyo, alisema masuala ya usajili amemuachia Mkurugenzi Mtendaji wa Man United, Ed Woodward. 

Griezmann bado ana mkataba na Atletico lakini inavyoonekana sasa uvumilivu unaanza kumshinda kutokana na presha kubwa ambayo amekuwa kiipata kutoka kwa mashabiki wa soka.
Ikumbukwe kuwa straika huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Atletico mwaka 2014 akitokea Real Sociedad, alifunga mabao 16 katika La Liga msimu huu uliomalizika wa 2016/17.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post