RAIS MAGUFULI AZIONYA KAMPUNI ZA SIMU NCHINI

SHARE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza taasisi za Serikali na taasisi binafsi zinazotumia mifumo ...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza taasisi za Serikali na taasisi binafsi zinazotumia mifumo ya kielektroniki kujiunga na mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki (Electronic Revenue Collection System {e-RCS}) ili kupata taarifa za uhakika na kulinda usalama wake pamoja na kuiwezesha Serikali kukusanya mapato yote stahiki.
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 01 Juni, 2017 alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (NationalInternetData Center) kilichopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam na kisha kuzindua mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki uliotengenezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kwa kutumia wataalamu wa ndani.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Tanzania Bara na Zanzibar na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka benki mbalimbali, kampuni za simu na viongozi wa dini.
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere kuwa mpaka sasa ni kampuni tatu za simu ambazo ni TTCL, Halotel na Smart ndizo zimejiunga kutumia Mfumo huu na kwamba TRA na ZRB zinatarajia kampuni zote za simu, mabenki na taasisi mbalimbali kujiunga na mfumo wa e-RCS kabla ya mwisho wa mwaka 2017.
“Wanaokusanya mapato wanalalamika kuwa kumekuwa na udanganyifu kwenye utoaji taarifa za wafanyabiashara na wafanyabiashara nao wanalalamika kuwa wamekuwa wakibambikizwa kodi, sasa dawa ya haya yote ni Kituo hiki cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu, jiungeni na mfumo huu kwa sababu sasa kila kitu kinafanywa na mashine, hakuna kuonea mtu, na Mhe. Makamu wa Rais naomba usimamie suala hili” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Pamoja na kutoa agizo hilo Mhe. Dkt. Magufuli ametaka taasisi zote za Serikali zenye vituo vya kumbukumbu (Data Centers) kuoanisha vituo hivyo na amepiga marufuku kuendelea kuanzisha vituo vingine, na badala yake zitumie Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzibana kampuni zote za simu ambazo hazijajiunga na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kujiunga haraka ili kuwepo uwazi katika uendeshaji wake huku akisisitiza kuwa Serikali inawapenda wawekezaji lakini ni lazima walipe kodi inavyostahili kwa ajili ya kujenga uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ameungana na Rais Magufuli kuzipongeza TRA na ZRB kwa kuanzisha mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki na amewataka Watanzania wote kulipa kodi ili kuinua uchumi.
“Natoa pongezi kwa kuanzishwa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu, kituo hiki ni ‘State of the Art’nakupongeza pia Mhe. Rais Magufuli kwa kuwa tangu uingie madarakani umetia msisitizo mkubwa katika kuongeza ukusanyaji wa kodi, na kwa kweli ukusanyaji wa kodi umeongeza” amesema Mhe. Rais Shein.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
01 Juni, 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: RAIS MAGUFULI AZIONYA KAMPUNI ZA SIMU NCHINI
RAIS MAGUFULI AZIONYA KAMPUNI ZA SIMU NCHINI
https://3.bp.blogspot.com/-gAp7xqOXT2g/WTBOwAHBP3I/AAAAAAAAcKQ/DmK3c-RPZPkiYQKAAYjJRbAtU2kQmH2qwCLcB/s1600/x2-2-750x375.jpg.pagespeed.ic.AU1Xud75Pt.webp
https://3.bp.blogspot.com/-gAp7xqOXT2g/WTBOwAHBP3I/AAAAAAAAcKQ/DmK3c-RPZPkiYQKAAYjJRbAtU2kQmH2qwCLcB/s72-c/x2-2-750x375.jpg.pagespeed.ic.AU1Xud75Pt.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/06/rais-magufuli-azionya-kampuni-za-simu.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/06/rais-magufuli-azionya-kampuni-za-simu.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy