REAL MADRID WAPIGA HODI KWA ROBERT LEWANDOWSKI

Real Madrid wanajipanga kumsajili supastaa wa Bayern munich Robert Lewandowski kwa mujibu wa chanzo cha Hispania.
Real Madrid wamejiwekea historia ya kuwa timu ya kwanza kutetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika zama hizi kwa kuipiga 4-1 Juventus katika fainali iliyochezwa mjini Cardiff, Juni 3, 2017.

Hata hivyo miamba hao wa Santiago Bernabeu bado wana nia ya kuzidi kuimarisha kikosi chao na wameshaweka bayana kwamba ni eneo gani wanataka kuliimarisha msimu ujao.

Kwa mujibu wa chanzo cha Hispania, Don Balon, Real Madrid wanajipanga kumsajili supastaa wa Bayern munich Robert Lewandowski. Ada inayokadiriwa kwa ajili ya mpachika mabao huyo wa Poland ni paundi milioni 97.

Zaidi ya hayo, ripoti zinadai kuwa Real Madrid watafanya jitihada kumsajili Lewandowski ikiwa Karim Benzema ataondoka klabuni hapo majira ya joto, jambo ambalo linawezekana sana kipindi hiki kutokana na kiwango dhaifu alichoonyesha msimu uliopita Santiago Bernabeu.

Lewandowski ni miongoni mwa wafungaji bora wa dunia, kuthibitisha hilo amefunga mabao 43 safi katika timu ya Bavaria katika michuano yote. Benzema kwa upande mwingine, amefanikiwa kufunga mabao 19 tu, ambapo 11 ni ya La Liga.

Zinedine Zidane anaweza kumpoteza Alvaro Morata, ambaye anakaribia kukamilisha dili la mamilioni ya paundi kutua Manchester United na ikiwa Benzema pia ataondoka, Madrid itakosa mshambuliaji mashuhuri.

Arsenal wanasemekana kuvutiwa na huduma ya Benzema na mshambuliaji huyo anaaminika kuwa tayari kutua Ligi Kuu Uingereza ili kupata uzoefu wa wa ligi ya nchi tofauti.

Imeripotiwa kuwa rais wa Real Madrid Florentino Perez ni shabiki mkubwa wa Lewandowski na anataka kumwona mchezaji huyo akishirikiana na Cristiano Ronaldo kuiongozea safu ya Los Blancos ya mashambulizi makali.

Real Madrid inawafuatilia kwa karibu Paulo Dybala, Kylian Mbappe na Pierre-Emerick Aubameyang PIA

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post