RIPOTI YA MCHANGA WA MADINI YAANZA KUIPA HASARA ACACIA KIMATAIFA

Jana hisa za kampuni ya kuchimba madini ya Acacia zilianza kuporomoka kwa zaidi ya asilimia 10 kwenye soko la hisa la jijini London, Uingereza baada ya jana Kamati ya Pili ya kuchunguza mchanga wa madini kutoa taarifa kuwa kampuni hiyo inafanya kazi nchini kinyume na Sheria za nchi kwakuwa haijasajiliwa hapa nchini lakini inafanya biashara ya matrilioni ya shilingi, kitendo ambacho ni sawa na kuiibia nchi.
Kamati hii ya pili ambayo jukumu lake ilikuwa ni kufanya tathmini ya athari za kisheria na kiuchumi kutokana na kampuni hiyo kusafirisha mchanga wa madini kwenda nje ya nchi ilibaini kuwa kampuni hiyo haijasajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA). Ripoti hiyo imeonesha kuwa kampuni ya Acacia haijawahi kupeleka nyaraka zozote zinazoonesha kampuni hiyo kumiliki au kuwa na hisa kwenye kampuni za uchimbaji madini za Bulyanhulu Mining ltd, North Mara Gold ltd au Pangea ltd.
Ripoti hii ya pili imekuja baada ya ripoti ya kamati ya kwanza iliyobaini kuwa kiwango cha madini kilichokutwa kwenye makontena yaliyozuiwa bandarini ni mara 10 zaidi ya kile kilichoandikwa kwenye nyaraka husika zilizowasilishwa kwenye mamlaka husika kwa ajili ya kuomba kibali cha kuyasafirisha.
Hadi saa tatu na nusu asubuhi ya jana, hisa za kampuni hiyo katika Soko la hisa la London zilikuwa zimeporomoka thamani kwa asilimia 14.
Hii ni sehemu ya taarifa iliyotolewa na kampuni ya Acacia: Tumethibitisha kuwa kamati hii ya pili imetoa taarifa yake kwa kutumia taarifa iliyotolewa na kamati ya kwanza iliyoundwa na Rais, iliyotolewa Mei 24, 2017 ambayo tunaipinga vikali.
“Taarifa ya kamati ya pili imesema kuwa tumedanganya taarifa zetu za mapato na kodi tunazolipa kwa miaka mingi na kutoa mapendekezo kadhaa yakiwemo kulipa malimbikizo ya kodi na mrabaha, kupitia upya mikataba ya uchimbaji mkubwa wa madini, Serikali kuwa na sehemu ya umiliki wa migodi yote na kuendelea kwa zuio la kusafirisha mchanga wa madini.
“Acacia tunapinga vikali shutuma hizi zisizo na msingi wowote. Tumekuwa tukiendesha shughuli zetu kwa kiwango cha hali ya juu na tunafata Sheria zote za Tanzania. Kwa mara nyingine tunasema kuwa tumekuwa tukitoa taarifa zote juu ya biashara tunayoifanya toka tuanze kufanya kazi nchini Tanzania na kwamba tumelipa pesa yote tuliyotakiwa kuilipa Serikali kama mrabaha na kodi stahiki katika madini yote tunayochimba ambayo tunatakiwa kulipia kodi. Pia, taarifa zetu za mahesabu huwa zinakaguliwa kila mwaka tena kwa kiwango cha kimataifa kwa kufuata masharti ya IFRS. (Shirika la Kimataifa la Viwango vya Ukaguzi wa Hesabu)
“Acacia tupo tayari kwa majadiliano na Serikali kuhusu swala hili na sisi pia tunajadiliana jambo sahihi la kufanya katika sakata hili na tutawataarifu kwa maamuzi yetu mapema iwezekanavyo.”
Zaidi, ili kutoa taarifa sahihi kuhusu sakata hili, tumetengeneza tovuti ndogo: http://www.acaciamining.com/export-ban-facts.aspx, ambapo tumeweka kumbukumbu toka kuanza kwa sakata hili, maelezo kuhusu shutuma hizi na taarifa kuhusu mchango wetu kwenye uchumi wa Tanzania.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post