SIFA ZA MUME WA MREMBO JOKATE MWEGELO

Kama wewe ni mwanaume na unatamani kumuoa mrembo maarufu nchini Tanzania, Jokate Mwegelo na unadhani kuwa itakulazimu uwe na fedha nyingi na handsome sana, hapo utakuwa umepotokana, kwani huo si mtazamo wa mrembo huyo.
Jokate Mwegelo amesema kuwa suala la fedha nyingi na mtu kuwa maarufu havina nafasi kubwa kwa mtu kuwa baba watoto wake, na hivyo akataja sifa ambazo yeye binafsi anazitaka.
Mrembo huyu ambaye anatamba pia na bidhaa zake za Kidoti amesema kuwa sifa za mwanaume ambaye anaweza kuwa mume, ni lazima awe na hofu ya Mungu na mwenye upendo wa dhati.
“Kusema kweli, kitu ninachotamani awe nacho mume wangi ni hofu ya Mungu. Mwanaume wa aina hiyo ni rahisi sana kumthamini mke wake.”
Jokate alisema kuwa kumtambua mwanaume mwenye upendo wa dhati si ngumu kwani unaangalia maisha yake binafsi lakini pia anaishije na ndugu, jamaa na rafiki zake.
Kuhusu suala la dini, Jokate alisema hilo si kikwazo kwake kwa sababu maisha yake yamezungukwa na watu wa imani tofauti tofauti, hivyo mwanaume wa dini yeyote ambaye anahofu ya Mungu anaweza kumuoa kwani anaamini hata wazazi wake hawatakaa.
Mrembo huyo hakuishia hapo kutiririka sifa za mwanaume anayetaka kumuweka ndani, kwani alisema jambo jingine ni uchapakazi na malengo yake ya siku za usoni.
Jokate aliweka wazi kuwa ndani ya miaka mitano ijayo anatarajia awe ameshaolewa na kuazisha familia yake ya watoto wasiozidi wanne.
“Familia ni jambo la muhimu, haya mambo tunayoyafanya sasa mwisho wa siku yatakwisha na umri unazidi kwenda, tutastaafu lakini familia itaendelea kuwepo. Nataka miaka mitano ijayo niwe mke wa mtu na mama wa watoto pacha,” alisema Jokate.
-Mwananchi
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post