SPORTPESA WAMSHUSHA BOSI WA EVERTON DAR, APOKELEWA NA WAZIRI MWAKYEMBE

Wengi watakuwa wanaifahamu Klabu ya Everton ya England, sasa habari ni kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Everton, Robert Elstone yuko  jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
Bosi huyo wa soka ametua nchini akiongozana na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Leon Osman ambapo wapo kwa ajili ya uzinduzi wa program za vijana kutoka kwenye akademi mbalimbali.

Ugeni wa Elstone umeratibiwa na kampuni ya kubashiri ya SportPesa na mgeni rasmi amekuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.

Ujio wa ugeni huo ni hatua chache kabla ya ujio wa timu ya Everton ambayo itakuja kucheza nchini mwezi ujao.

Kwenye shughuli hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa asubuhi ya leo pia alikuwepo Ofisa Mtendaji Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov.

Bosi huyo wa Everton amepata nafasi ya kuwaona watoto na vijana wa Kitanzania wakicheza soka kwenye Uwanja wa Taifa.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post