VANESSA MDEE AWAKOMESHA WALIOKUWA WAKIMSEMA JUX

Mwanamuziki Juma Jux ukipenda muite African Boy, leo amehitimu masomo yake nchini China ambapo ametunukiwa Shahada ya Awali (Bachelor Degree) katika masomo ya Sayansi ya Kompyuta (Computer Science) kutoka Chuo Kikuu cha Guangdong nchini China.
Kwa muda mrefu watu mbalimbali wamekuwa wakihoji kuwa Jux anafanya nini China huku wengine wakidiriki kusema kuwa alikuwa akijihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa sababu hawakuwahi kuona hata picha yake akiwa darasani ili kuthibitisha aliyokuwa akiyasema kuwa anasoma.
Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram, Jux amesema kuwa katika miaka minne aliyokuwa akisoma alikumbana na vikwazo vingi ambavyo vilikaribia kumkatisha tamaa lakini baadhi ya watu walimtia moyo na leo amehitimu.
Mbali na Jux, mpenzi wake, Vanessa Mdee ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akimsifia kuwa afadhali amemaliza na picha zake sasa zimeonekana kwa sababu watu walikuwa wakiuliza maswali mengi kuwa anafanya nini China.
“Congratulations @juma_jux U finally done ✅ and you done did it well. Hapo watu walikuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii picha jibu la kutosha.”
Mbali na hilo, Vanessa amempongeza Jux kwa kufanikiwa kufanya kwa pamoja, muziki, biashara na bado akaweza kuzingatia masomo yako jambo ambalo huwashinda watu wengi.
“Umeweza kufanya yote, MZIKI, BIASHARA NA SHULE… now that’s exceptional. Muda wa vibunda babaaa. Keep inspiring the YUTEEEEE 🙌🏾👌🏾🎊
Hapa chini ni baadhi ya picha za Jux katika mahafali hayo.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post