VIDEO: MCHEZAJI TIGER WOODS AKIPIMWA ULEVI KWA KUTAKIWA KUTEMBEA JUU YA MSTARI WA BARABARA

Jeshi la Polisi katika Jimbo la Florida wamechapisha video ya gwiji wa mchezo wa Gofu nchini Marekani, Tiger Woods akipata shida kutembea juu ya mstari katikati ya barabara katika kile kilichoelezwa alikuwa akipimwa kama amelewa baada ya kukutwa akiwa amelala kwenye gari.
Mwanamichezo huyo alikamatwa siku ya Jumatatu ambapo amesema kuwa ulevi haukuwa sababu ya yeye kukamtwa. Baada ya kukamtwa alishtakiwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa lakini yeye alisema alipata matatizo kutokana na dawa alizomeza, ila haikuwa pombe.
Nataka umma ujue kwamba sikuwa nimelewa, lakini tatizo lilitokana na dawa nilizokuwa nimetumia kabla ya kuendesha gari, alisema Tiger Woods.
Mkanda wa video uliotolewa na Polisi unamuonyesha Tiger akitakiwa kutembea katikati ya mstari wa barabara, ili kuonyesha kama kweli alikuwa akiendesha gari chini ya nguvu ya pombe au la.
Hapa chini ni video hiyo;

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post