VIDEO: TAARIFA YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU SAKATA LA MCHANGA WA MADINI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji hasa kwenye sekta ya madini na watanzania kwa ujumla kuwa wavumilivu kuhusu suala la mchanga wa madini hadi hapo ripoti kamili itakapokamilika ili maamuzi yatolewe.
Wazir Mkuu alisema kuwa hadi sasa hakuna maamuzi yoyote yaliyochukuliwa na serikali kuhusu ripoti ya kwanza iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli na Prof. Mruma zaidi ya kuwawajibisha wale waliokuwa na dhamana ya kusimamia rasilimali hiyo.
Hayo yalisemwa na kiongozi huyo wa shughuli za serikali wakati akijibu swali la Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini kwa tiketi ya CCM aliyetaka kujua serikali inatamka nini kuwaondolea hofu wawekezaji kwenye sekta ya madini kufuatia mchanga wa madini wa Acacia kuzuiliwa kusafirishwa nje.
Watanzania na pia wabunge katika michango yenu ya kipindi cha nyuma, mlikuwa mnaitaka serikali ichunguze mchanga wa madini unaosafirishwa kwenda nje, na Rais wetu Dkt Magufuli ametekeleza hili, alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alilieleza Bunge kuwa lengo la serikali ni kujua huo mchanga unaosafirishwa nje una nini, na si kweli kwamba wanakusudia kuzuia uchimbaji huo.
Kwa sasa tunasubiri taarifa ya kamati ya pili. Baada ya hapo serikali itakaa chini, itatafakari, itapata ushauri kutoka sekta mbalimbali za kiuchumi na kisheria, kuhusu hatua gani zichukuliwe, alisema Waziri Mkuu.
Hapa chini video ya Waziri Mkuu akitolea ufafanuzi suala hilo;JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post