WABUNGE WA UPINZANI WATOKA NJE WAKIPINGA UAMUZI WA SPIKA WA BUNGE

Mbunge wa upinzani wametoka nje ya ukumbi wa bunge wakati kikao cha bunge kikiendelea wakipinga uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kuamuru Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kutolewa nje kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Spika wa Bunge ametoa maamuzi ya kutolewa nje kwa Mnyika baada ya kudaiwa kuonyesha vitendo visivyo vya kibunge wakati mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini ukiendelea. Spika alisema Mbunge huyo asingeruhusiwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa wiki moja.
Wakiwa nje ya ukumbi wa bunge, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya alizungumza na waandishi wa habari na kusema hawakubaliani hatua iliyochukuliwa na spika dhidi ya mwenzao kwani kuna mbunge wa CCM alisema wabunge wengine hawana akili lakini hakuchukuliwa hatua yoyote.
“Nadhani hata nyinyi mmeona mbunge aliyekuwa anachangia anasema kuwa wabunge wengine wapimwe akili, inawezekana hawana akili anaachwa kwa sababu tu ni mbunge wa Chama Cha Mapinduzi.”
Aidha, Bulaya alisema kazi ya upinzani ni kuikosoa serikali pale mambo yanapokuwa hayaendi sawa ni si kupongeza kila kitu. Alifafanua zaidi kuwa hawawezi kuwa wanaisifia tu serikali, bali watafanya hivyo pale panapopasa kama kwenye wizara ya ardhi ambapo walimpongeza waziri kwa kazi kubwa anayofanya.
“Msimamo wetu kama Kambi ya Upinzani tumeamua kutoka kwa sababu hatuwezi kujadili mambo ya msingi kwa kufanyiwa mambo haya, sisi kazi yetu ni kuishauri serikali lakini hatuwezi kuishauri serikali vile wanavyotaka wao. Kwenye Wizara ya Ardhi mbona wabunge wa upinzani walisimama na wakapongeza na Wizara ya Ardhi ilipita bila shida yoyote kwa pande zote mbili, sasa kwanini wao wanataka kupongezwa tu? Kazi yetu ni kuona pale ambapo mambo hayaendi sawa kwa mujibu wa sheria tunasema na hili liwe wazi watu waliokuwa wakipigia kelele mikataba mibovu ni upinzani bungeni” alisisitiza Ester Bulaya.
Wakati huo huo, Kamati ya Bunge ya Maadili itamjadili Mbunge Esther Bulaya kwa kosa la kushawishi wenzake kutoka nje.
Spika wa Bunge pia ameiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujadili kitendo cha Mbunge wa Kawe, Halima Mdee cha kuzuia Askari wa bunge kumtoa nje Mbunge John Mnyika.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post