WACHEZAJI SITA WAPYA KWENYE KIKOSI CHA AZAM FC MSIMU WA 2017/18

SHARE:

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuwataarifu wapenzi na mashabiki wa soka nchini kuwa imebadilisha ...

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuwataarifu wapenzi na mashabiki wa soka nchini kuwa imebadilisha mfumo wa usajili uliokuwa ikiutumia awali wa kusajili wachezaji kwa gharama kubwa na sasa ikijikita kwenye kufanya matumizi ya wastani pamoja na kuwatumia ipasavyo nyota watakaozalishwa kutoka kituo chao ‘Azam Academy’.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd, leo imeeleza kuwa kuelekea msimu ujao na kuendelea, Azam FC itaweka msisitizo na kufanya uwekezaji ipasavyo kwenye kituo chake cha kukuza vipaji ‘Azam Academy’ ili kuvuna wachezaji bora watakaopandishwa katika kikosi cha timu kubwa.
Kwa kuanzia katika kutekeleza malengo hayo, kuelekea msimu ujao Azam FC imewapandisha wachezaji sita kutoka kwenye kituo chake, ambao ni mabeki Abbas Kapombe, Abdul Haji, Godfrey Elias, kiraka Ramadhan Mohamed, kiungo Stanslaus Ladislaus na mshambuliaji Yahaya Zaid, aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Daraja Kwanza (FDL) msimu uliopita kwa mabao 12 aliyofunga alipokuwa kwa mkopo Ashanti United.
Azam FC imekuwa na utaratibu mzuri wa kulea wachezaji wake vijana kwa kuwapandisha kwenye timu kubwa, ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuibeba timu, ambapo wengine waliopo katika kikosi cha wakubwa ni makipa Aishi Manula, Metacha Mnata, mabeki Gadiel Michael, Ismail Gambo, kiungo Mudathir Yahya, Abdallah Masoud, Himid Mao, Joseph Mahundi na mshambuliaji Shaaban Idd.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, aliyeongezewa mkataba wa mwaka mmoja, anaamini ya kuwa wachezaji hao vijana watazidi kukiimarisha kikosi chake kwa kushirikiana na wachezaji wazoefu waliopo kikosini, hadi anafikia uamuzi huo wa kuwapandisha aliwafuatilia katika mechi mbalimbali za timu ya vijana ikiwemo na baadhi ya siku kuwajumuisha katika mazoezi ya timu kubwa.
Aidha kuhusiana na wachezaji waliomaliza mikataba yao, Azam FC imethibitisha rasmi kuachana na winga wake Khamis Mcha ‘Vialli’ na Ame Ally, aliyekuwa kwa mkopo Kagera Sugar, wote mikataba yao ikiwa imemalizika.
Mabadiliko kwenye mfumo wa uongozi
Katika hatua nyingine, Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC imefanya mabadiliko ya mfumo wa kiuongozi ya timu hiyo kwa kukifuta cheo cha Ofisa Mtendaji Mkuu, na sasa cheo cha juu kitakuwa ni Meneja Mkuu, nafasi inayoshikiliwa na Abdul Mohamed.
Kutokana na mabadiliko hayo ya kiutendaji, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, amemaliza mkataba wake na pande zote mbili zimekubaliana kuachana, na sasa majumuku yake yote yatafanywa na Abdul Mohammed, akiwa ndio Meneja Mkuu wa klabu.
Timu kuanza mazoezi Julai 3
Katika hatua nyingine, Alando aliweka wazi kuwa kwa sasa timu ya wakubwa ipo mapumziko kwa takribani wiki tano baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi na kitarejea tena mazoezini Julai 3 mwaka huu, tayari kabisa kuanza maandalizi ya msimu ujao 2017/2018.
Alisema kwa sasa wapo kwenye harakati za kuifanyia kazi ripoti ya kocha wao likiwemo suala la usajili, ambapo amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa tayari wameshafanya mazungumzo na wachezaji wanaowahitaji kwa ajili ya msimu ujao.
“Kwa wachezaji ambao wanatoka nje ya Azam ambao ni wa Kitanzania, hatuko tayari kuweka majina wazi hivi sasa, lakini kuna watu tumeshafanya nao mazungumzo, kuna watu tayari tunaelekea kumalizana nao, uongozi unajua nini unachofanya, hivyo napenda kuwaambia Watanzania usajili unaendelea chini kwa chini na hii ni vita, pale ambapo tutakuwa tumemalizana na mchezaji fulani tutaweka wazi,” alisema.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WACHEZAJI SITA WAPYA KWENYE KIKOSI CHA AZAM FC MSIMU WA 2017/18
WACHEZAJI SITA WAPYA KWENYE KIKOSI CHA AZAM FC MSIMU WA 2017/18
https://3.bp.blogspot.com/-5CK8jJEOXDs/WTGuWKwYAYI/AAAAAAAAcLg/L_M0zf0CvYYSOtzA7P62S3aUs1b0MdHUgCLcB/s1600/xIMG_1784_0-750x375.jpg.pagespeed.ic.d3Nahy_k8P.webp
https://3.bp.blogspot.com/-5CK8jJEOXDs/WTGuWKwYAYI/AAAAAAAAcLg/L_M0zf0CvYYSOtzA7P62S3aUs1b0MdHUgCLcB/s72-c/xIMG_1784_0-750x375.jpg.pagespeed.ic.d3Nahy_k8P.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/06/wachezaji-sita-wapya-kwenye-kikosi-cha.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/06/wachezaji-sita-wapya-kwenye-kikosi-cha.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy