WANANCHI WAMTAKA MBUNGE WAO AJIUZULU KWA KUHUSIKA NA MCHANGA WA MADINI

Baadhi ya wananchi wa Igunga mkoani Tabora wamemshauri Mbunge wao, Dk. Peter Kafumu kujiuzulu kwa madai ya kushindwa kutumia madaraka yake vizuri alipokuwa Kamishna wa Madini.
Wananchi hao walionyesha kusikitishwa na taarifa mbili za kamati zilizoundwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga wa madini ya dhahabu ambao husafirishwa nje ya nchi kwa lengo la kwenda kuchenjuliwa ili kupata mdini yaliyondani.
Dk. Peter Kafumu.
Baadhi ya waliotoa maoni kuhusu ushauri huo kwa mbunge wao, walisema kuwa ni vyema akaachia ngazi kwani haitamanisha kwamba ameshindwa bali ni uwajibikaji.
Oscar Thomas alisema akiwa mmoja wa wapiga kura, ameona ni vema mbunge wao akajiuzulu   kwa kuwa yeye ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kuilingizia taifa hasara kwa kushiriki kutengeneza mikataba mibovu ya madini.
Kwa upande wake Thomas alisema, kazi anayofanya Rais Magufuli ya kufuatilia rasilimali za nchini anapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mwenye uchungu na taifa hili lakini pia viongozi walioingia mikataba hiyo wanatakiwa wachukuliwe hatua.
Mbali na Kafumu kushiriki katika mkataba ya madini ambayo inadaiwa kuliingizia taifa hasara ya trilioni 108, Rais Magufuli alimtuhumu kuwa alitaka kuishawishi kamati ya kwanza ili kubadilisha ripoti waliyoiwasilisha kwa Rais.
Wananchi wa Igunga wamemtaka Rais Magufuli kutokatishwa tamaa na baadhi ya watu wanaopinga juhudi zake za kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinawanufaisha watanzania.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Igunga, Costa Ollomi  na Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mwanamvua Killo wamesema kazi anayoifanya Rais Magufuli imeleta heshima ndani ya chama na serikali.
Kuhusu wananchi kumtaka mbunge wao kujiuzulu ubunge alisema yeye hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa tayari Rais alikwisha kutoa maelekezo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post