YANGA VS WAKENYA UWANJANI LEO, MWAMBUSI AWAITA MASHABIKI WAKASHUHUDIE VIPAJI

Mechi za nusu fainali za michuano ya SportPesa Super Cup zinatarajiwa kuchezwa leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Uhuru.
SportPesa Super Cup ni michuano mipya ambayo ilianza Jumatatu ya wiki hii na kuhsuhudia wachezaji wengi wageni wakizitumikia timu shiriki huku Simba ikiondolewa mashindanoni kwa penalti.
Timu zilizopata nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya SportPesa Super Cup ni Yanga, Gor Mahia, AFC Leopards ‘Ingwe’ na Nakuru All Stars zote za Kenya.

Kuelekea mchezo dhidi ya AFC Leopards, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa kikosi chao kipo fiti na kuwataka mashabiki wao kufika kwa wingi uwanjani kushuhudia mchezo huo ambapo wataona vipaji vipya vya timu yao.

“Tupo tayari na mashabiki wafike kwa wingi kwa kuwa una vijana wengi ambao tunatarajia kuwapa nafasi ya kucheza kwa kuwa baadhi ya wachezaji hawapo. 

“Hivyo, mashabiki waje waishuhudia Yanga ijayo,” alisema Mwambusi.

Mchezo mwingine wa nusu fainali, Nakuru All Stars itakuwa na kibarua mbele ya Gor Mahia.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post