YASEMWAYO MITANDAONI BAADA YA RAIS MAGUFULI KUMTEUA ANNA MGHWIRA KUWA RC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amemteua Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Rais Magufuli amefanya uteuzi huo ambapo Mghwira anachukua nafasi ya Said Meck Sadick aliyeandika barua kwa Rais akiomba kujiuzulu mwezi Mei mwaka huu.
Uteuzi huo umemkuta mwenyekiti wa ACT Wazalendo akiwa katika kongamano la chama hicho lililokuwa likijadili sakata la kuzuiwa kwa mchanga wa madini kusafirishwa kwenda nje. Hadi sasa chama hicho na mteule hawajatoa taarifa yoyote kuhusu uteuzi huo.
Watu mbalimbali kupitia mitandao wametoa maoni yako kuhusu uteuzi huo, jambo kubwa likiwa ni kwa namna gani kiongozi huyo atakwenda kutekekeleza ilani ya Chama cha Mapainduzi. Wengi waliotoa maoni walisema kuwa, Mkuu wa Mkoa ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na mjumbe wa vikao vya CCM Mkoa, hivyo swali linakuwa, je! Anna Mghwira ambaye ni mwanachama wa ACT Wazalendo, ataingia kwenye vikao vya CCM?
Hapa chini ni maoni ya baadhi ya watumiaji wa mitandao kuhusu uteuzi huo. Na wewe unaweza kuandika maoni yako chini mwishoni mwa habari hii.


Katiba Inasema Mkuu wa Mkoa ambaye ni mwanachama kumbe kuna Ambaye Siye mwanachama ....Haihitaji Degree ya Sheria
Kuona hili
Hongera sana mama ๐Ÿ‘๐Ÿ‘kwa kuteuliwa na Rais kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nakuamini sana ๐Ÿ™‹… https://www.instagram.com/p/BU4gbVQF1k1/ 
Mkuu wa Mkoa ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na mjumbe wa vikao vya CCM Mkoa! Je, Anna Mwigira atakuwa anahudhuria vikao vya ccm?
Sasa Wabunge wa CCM wajifunze kutoka kwa Mheshimiwa Rais. Wakati yeye anaona karama ya Uongozi kwa Upinzani, Wabunge CCM wafuate nyayo hizo
Kwa maana hiyo Chama Cha Mapinduzi hakina mwanachama ambaye ataweza kuwa Mkuu wa Mkoa?๐Ÿ˜‰
Kitila katibu wa wizar ya maji anna mwingira mkuu wa mkoa wa kilimanjaro kwa maana @ACTwazalendo kuna viongozi makini soon @zittokabwe
Sio tu kawa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro; bali pia mjumbe wa kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro! @zittokabwe @Chahali
Kitila ACT :katibu Mkuu wizara ya maji
Anna mgwira ACT :Mkuu Wa mkoa Kilimanjaro
Zitto kabwe ACT :Waziri Nishati na madini. End of story.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro kwenye majukumu yake atatumia ILANI ipi sasa?ya chama chake au tawala?Bado NAWAZA ๐Ÿค”

Kwa Mujibu Wa Katiba Ya Chama Chetu, Mkuu Wa Mkoa Ni Mjumbe Wa Kamati Ya Siasa Ya Mkoa, Hongera Anna Mgwira Na Karibu CCM !!


Itakuwaje Mama Mghwira atakapopewa "maelekezo kutoka juu" kuzuwia mkutano wa Zalendo mkoani mwake? 
ACT nd'o imeisha hivo...Kitila kachukuliwa, Msando kachukuliwa na Gigy...Anna Mghwira naye kachukuliwa...kabaki Zitto peke yake๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Naendelea kumtia moyo @zittokabwe asivunjike moyo hata kama utalazimishwa kupita kwenye mteremko wenye utelezi mkali. Keep doing what you do




JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post