YASEMWAYO MITANDAONI KUHUSU WANAFUNZI WENYE MIMBA KUTORUDI SHULENI

Wananchi wameipokea kwa namna mbalimbali kauli ya Rais Magufuli aliyoitoa jana kuhusu watoto wa kike wanaopata mimba wakiwa shule ambapo alisema, chini ya utawala wake, hakuna mwanafunzi atakayerudi shule baada ya kujifungua.
Rais Magufuli aliitoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia wananchi wa Bagamoyo baada ya kuwepo kwa watu mbalimbali hasa asasi za kirai na wanaharakati wa haki za wanawake wakitaka watoto wa kike waruhusiwe kurejea shule baada ya kujifungua.
Wanaharakati hao wamesema kuwa idadi ya wanafunzi wanaopata mimba ni kubwa sana hivyo kusema wasirejee shule ni kuendeleza kutengeneza jamii yenye wanawake ambao hawana elimu na hivyo kuzidi kufanya harakati za kufikia 50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake kuwa ngumu.
Kwa upande wake Rais Magufuli alisema, serikali yake haiwezi kutoa fedha kwa ajili ya kuwasomesha, wakapate mimba alafu isomeshe wazazi. Lakini pia alisema ukiwaruhusu warudi shule, itapelekea wanafunzi wengi kujiingiza katika vitendo vya ngono na kubeba ujauzito kwa sababu wanajua watarudi shule.
Mvutano baina ya pande hizo mbili umeendele kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vijiwe vya kupiga soga kila mmoja akivutia upande wake. Hapa chini ni maoni ya baadhi tu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wakisema mawazo yao;
Takwimu za mimba za utotoni zimepanda kutoka 24% - 27% mwaka Jana.Kila mwaka wasichana 30 kati ya 100 wanaacha shule sababu ya mimba (TDHS)
Lazima tujenge jamii yenye maadili bora kuanzia watoto mpaka wazee.Binti akipata mimba wakati bado anasoma hatakiwi kurudi shule,thats it
My TL is depressing i can't believe TZ kuna misogyny kiasi hichi! Statements zinzaoongelewa kuhusu watoto wa kike utashangaa. Tumerudi nyuma
Maamuzi haya yataathiri zaidi wasichana wanaotoka kwenye familia maskini,ambao ndio wengi.Very saddened by this statement 
3,400+ girls dropped out of school in Tanzania last year because of pregnancy. Boys, zero. And we don't see anything wrong with this.

Elimu haibaguwi
Rashida wala Rashidi
Pili wala Zitto
Mzazi wala mjamzito
Elimu ni utu
Wa kila Mtu
Ni ubinadamu
Wa MwanaWaAdamu
Ukimpa mwnfunz mimba jela miaka 30 mama anafukuzwa shule baba yuko jela mtoto huyu nae itakuwa ngumu pia kuepuka mimba ya utotoni# mzunguko
Kila mtu Ana haki ya kupata elimu na kila raia Ana haki ya kujielimisha Kwa kadiri ya uwezo wake katika nyanja achaguayo- Katiba JMT 11(2)
Ni marufuku mtu yeyote au mamlaka yeyote kubagua mtu mwengine chini ya sheria yeyote au katika utendaji wowote wa dola- Katiba JMT 13(4)(5)
Tunavyolazimisha kuwahukumu wanafunzi kwa kubeba ujauzito utadhani watoto wa kike wanaenda kuzinunua mbegu za kiume supermarket.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post