ABDI BANDA AONDOKA TANZANIA KWENDA

Hatimaye beki wa Simba Abdi Banda ameondoka nchini kuelekea Afrika Kusini kujiunga na timu yake mpya Baroka FC.
Banda ametoa somo kwa wachezaji wa Tanzania ambao wanatamani kupata nafasi ya kucheza nje ya nchi kwamba wakipata nafasi wasiangalie nyuma wazitumie haraka iwezekanavyo kutoka.

“Wachezaji wajitume na wanatakiwa kuwa makini na nafasi, zinapotokea nafasi za kutoka kwenda kucheza nje ya nchi, wasiangalie nyuma wazitumie nafasi hizo,” – Abdi Banda.

“Tunahitaji timu ya taifa nzuri, bila wachezaji wengi kucheza nje ya Tanzania hatuwezi kupata timu nzuri ya taifa. Kikubwa ni kuongeza juhudi na kufanya mipango ili wachezaji wengi tucheze nje ya nchi.”

Banda tayari alishasaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo wakati akiwa kwenye michuano ya COSAFA Cup 2017 mashindano ambayo yamemalizika Afrika Kusini huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post