AMBER LULU HATASAHAU KUCHANGIA PENZI NA GIGY

Gigy Money.

MUUZA sura kwenye video za Kibongo ambaye kwa sasa anatamba na Wimbo uitwao Watakoma, ‘Amber Lulu’amefunguka kuwa katika mambo ambayo hawezi kuyasahau kwenye maisha yake ya uhusiano wa kimapenzi ni kitendo cha kuchangia penzi la mwanaume mmoja na mwanamuziki mwenziye Gigy Money.
Amber Lulu.
Akizungumza na Uwazi Showbiz, Amber alisema kuwa kitendo hicho kilimuuma sana ukizingatia Gigy ni mtu wake wa karibu lakini hata baada ya kugundua kuhusu hilo hakuweza kugombana na Gigy kwa sababu hata yeye hakuwa anafahamu kuwa alikuwa ni mpenzi wake.
“Tulichokifanya ilikuwa ni kuachana na mwanaume huyo ambaye ni mtangazaji wa kituo kimoja cha televisheni nchini na kila mmoja wetu akatafuta mwanaume mwingine maana tuliona hatufai, alituchanganya wakati akifahamu sisi ni marafiki,” alimaliza Amber Lulu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post