ANACHOKIPENDA CHEMICAL KUTOKA KWA DAVIDO

Msanii wa Bongo Fleva, Chemical ameeleza kuwa hit song ya Davido ‘If’ ni moja ya vitu anavyovipenda kwa sasa kutoka kwa msanii huyo wa Nigeria.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Queen of Dar es Salaam’, ameiambia Clouds FM Top 20 kuwa Davido ana muziki wake wa asili licha ya kuwa ni msanii wa kisasa.
“If ni ngoma ambayo mwenyewe naipenda, nampenda Davido kwa hiyo If ni ngoma nzuri. Davido ni mtu ambaye sidhani kama ameshawahi kutoa ngoma mbaya halafu anajaribu kuweka ID yao katika ngoma zake, ni mnyamwezi lakini anaweka vitu fulani ambavyo utatamani kujua maana yake na mtu utapenda kusikiliza kwa sababu ya melody na vitu vingine vya kimuziki,” amesema Chemical.
By Peter Akaro
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post