ARSENAL YAMPA ‘MAKAVU’ SANCHEZ, YAMWAMBIA HAIWEZI KUMRUHUSU ATUE MANCHESTER CITY

Klabu ya Arsenal imepanga kumwambia mchezaji wake, Alexis Sanchez kuwa haitaweza kumuuza kwenda Manchester City, kama ambavyo imekuwa ikidaiwa kuwa anaweza kwenda huko.
Mchezaji huyo inaaminika kuwa anaweza kuondoka Arsenal ili kwenda kuungana na kocha wake wa zamani Pep Guardiola ambaye waliwahi kufanya naye kazi pamoja Barcelona.

Amekuwa akitajwa kuwa anaweza kondoka Arsenal kutokana na kutokubaliana na klabu yake hiyo katika masuala ya kifedha hasa kuhusu mshahara ambapo mbali na Man City, pia amekuwa akiwaniwa na Paris Saint-Germain na Bayern Munich.

Hivi karibuni Sanchez alinukuliwa akisema tayari ameshajua juu ya mwelekeo wake lakini hawezi kusema kwa sasa.

Ili kuziba pengo lake ikiwa ataondoka klabuni hapo, tayari Arsenal imeanza mchakato wa kumuwania Kylian Mbappe wa Monaco pamoja na Alexandre Lacazette wa Lyon.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post