ASKOFU GWAJIMA AUGUA KESI YAKE IKIENDELEA MAHAKAMANI

Hukumu ya kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha inayomkabili Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Gwajima imeahirishwa kutolewa leo Julai 31, 2017 na badala yake itatolewa Agosti 30 mwaka huu.
Kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha imeahirishwa leo kutokana na hakimu hiyo kupata udhuru pamoja na Askofu Gwajima kuwa mgonjwa na hivyo kushindwa kufika mahakamani.
Wakiwa mahakamani hapo leo, wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro aliiambia mahakama kwamba, washtakiwa George Mzava, Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze (39) na Georgey Milulu wapo mahakamani lakini Askofu Gwajima hayupo na hivyo wakili wa Gwajima akalazimika kueleza sababu.
Akijibu madai hayo, Wakili Peter Kibatala ambaye ndiye anamtetea Askofu Gwajima na wenzake watatu alimweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wakati kuwa Askofu Gwajima ni mgonjwa na amewakilishwa mahakamani hapo na mdhamini wake.
Baada ya maelezo hayo kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 30 mwaka huu.
Katika kesi ya msingi, Mzava, Bihagaze na Milulu wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki bastola aina ya berretta pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post