ATUPWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA NA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 8- ROMBO

SHARE:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili ndg Benedict Joachim Kimario (46) ambaye ni mzali...

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili ndg Benedict Joachim Kimario (46) ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Mrao Kata ya Mraokeryo iliyopo Tarafa ya Mashati wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, ambapo alikuwa akituhumiwa kwa kumbaka na kumlawiti mtoto Lucia Faustini Kitalala (08) ambae ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mkovanda wilayani humo.
Akisoma hukumu hiyo mbele ya mahakama ya hakimu mkazi mkoani humo, hakimu Aidadi Hendry Mwilapwa amesema kuwa mtuhumiwa atakwenda kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kutenda makosa mawili tofauti ambayo ni ubakaji na kosa la kulawiti. Makosa hayo kila moja limetolewa hukumu yake kulingana na sheria za nchi ambapo kulingana na uzito wa makosa hayo mahakama imetoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini wilayani Mererani mkoani Arusha.
Inaelezwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo tarehe 10/05/2016 ambapo alimbaka na kumlawiti mtoto huyo na kisha kukimbilia Mererani kabla ya kutiwa nguvuni na jeshi la polisi wakishirikiana na Diwani wa Kata ya Mraokeryo, Athuman Kimario.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo mapema leo Diwani wa Kata ya Mraokeryo, Athuman Kimario, amesema kuwa kesi hii imechukua muda mrefu lakini anaishukuru mahakama kwa kutenda haki.
“Kesi hii imechukua muda mrefu kwa kweli lakini leo hii mahakama imetenda haki na hii itakuwa fundisho hasa kipindi hiki ambacho matukio ya ubakaji na ulawiti yanazidi kupamba moto katika kata yangu”
Amesema diwani huyo na kuongeza kuwa atahakikisha kuwa mtu yeyote atakaejihusisha na vitendo vya ubakaji na ulawiti katika kata yake anaripotiwa kwa vyombo husika ili hatua kali zichukuliwe dhidi yake na hatimae iwe ni mwarubaini wa tatizo hilo kwenye kata yake.
Aidha, wazazi wa mtoto Lucia mbali na kuishukuru mahakama kwa kutenda haki, wamempongeza diwani huyo na kumtaka aendelee na uwajibikaji na weledi aliouonesha kwenye kesi dhidi ya mtoto wao.
Hukumu ya mshtakiwa Benedict imekuja wakati ambao mkazi mwingine wa kata hiyo anayefahamika kwa majina ya Amedeus Clemens akishikiliwa na jeshi la polisi kufuatia kutuhumiwa kumbaka na kumlawiti mtoto wa miaka minne ambae naye ni mkazi wa kata hiyo.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: ATUPWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA NA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 8- ROMBO
ATUPWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA NA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 8- ROMBO
https://3.bp.blogspot.com/--sNm7VCFY2E/WXJhTQE-RaI/AAAAAAAAc54/2y988zaGywUWjZFYJrfshGhUwaeM5NlRwCLcBGAs/s1600/x183890188-612x375.jpg.pagespeed.ic.c3z9xc9tsa.webp
https://3.bp.blogspot.com/--sNm7VCFY2E/WXJhTQE-RaI/AAAAAAAAc54/2y988zaGywUWjZFYJrfshGhUwaeM5NlRwCLcBGAs/s72-c/x183890188-612x375.jpg.pagespeed.ic.c3z9xc9tsa.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/atupwa-jela-maisha-kwa-kumbaka-na.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/atupwa-jela-maisha-kwa-kumbaka-na.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy