BAFANA BAFANA Vs TAIFA STARS MZIGONI LEO ROBO FAINALI YA COSAFA

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajiwa kukipiga na wenyeji Afrika Kusini katika michuano ya Kombe la Cosafa, leo Jumapili, mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng, Rusternburg, Afrika Kusini.
Afrika Kusini maarufu kwa jina la Bafana Bafana ndiyo wenyeji wa michauno hiyo na mchezo huo utakuwa ni wa Robo Fainali ya Cosafa na utaanza saa kumi na mbili kamili jioni kwa muda wa Afrika Mashariki.
Bafana Bafana imeanzia moja kwa moja hatua hiyo, wakati Taifa Stars imefika hapo baada ya kuongoza Kundi A katika hatua ya awali, ikitoa sare mbili, 1-1 na Mauritius na 0-0 na Angola baada ya kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza na Malawi.
Tanzania ikaipiku Angola kwa wastani wa mabao baada ya kulingana nayo kwa pointi, huku timu nyingine katika kundi hilo, Mauritius na Malawi zote zikimaliza na pointi mbili kila moja.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga japokuwa atamkosa beki wake wa kati Abdi Banda anayetumikia adhabu ya kadi za njano, lakini hana wasiwasi kwa sababu anaamini pengo hilo litazibwa.
Kocha wa Afrika Kusini, ambao ni mabingwa watetezi Stuart Baxter anataka kuitumia mechi hiyo kuwajaribu baadhi ya wachezaji ambao hawajawahi kupata nafasi timu ya taifa.
Utakuwa mchezo wa kwanza Bafana Bafana kumenyana na Tanzania, wageni waalikwa kutoka Afrika Mashariki kwenye michuano hiyo ya nchi za Kusini mwa Afrika tangu mwaka 2011 kocha wa wakati huo, Pitso Mosimane alipopeleka kikosi Dar es Salaam kwa mchezo wa kirafiki na kushinda 1-0, bao pekee la Siyabonga Sangweni Mei 14 Uwanja wa Taifa.
Kwa ujumla, timu hizo leo zinakutana kwa mara ya tatu, baada ya awali kabisa katika michuano ya CECAFA Castle Oktoba 26, mwaka 2002 na wenyeji Tanzania wakashinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post