BAMBO ATOA YA MOYONI, WACHEKESHEJI KULIPA KODI

Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini Tanzania anayefanya vizuri kwa sasa katika kipindi cha Ze Comedy ameshitushwa na mpango wa Serikali wa kutaka washereheshaji wa harusi (Ma-MC) kulipa  kodi.
Akizungumza katika mahojiano na  Sasa Tv nyumbani kwake jijini Dar es salaam Bambo alisema Serikali iangalie jambo hilo kwa mapana zaidi  ili lisije kuwaumiza Ma Mc katika utekelezaji wa kazi zao.
“Ni haki kwa kila Mc kulipa kodi ili kujenga nchi ila tuwekewe mazingira bora na yenye tija kwani kazi zenyewe zinapatikana kwa msimu lakini kama tutakuwa tunapata na zile za Serikali mtu anajua kwa mwezi atafanya kazi hata tatu hivyo hawezi pinga kulipa kodi” Alisema Bambo.
“Unakuta mc anapata sherehe tatu kwa mwezi na zote wanamuomba na kumbembeleza pengine hata malipo yenyewe yanasua sua ingawa wapo washereheshaji wengine wanalipwa mpaka milioni tano kwa tukio lakini sio mara kwa mara.”aliongeza Bambo
Bambo  amewaomba   washehereshaji wenzake  wajitokeze kwa wingi katika kujadili na kupata suluhu suala la kulipa kodi ili washirikiane kwa pamoja katika kujenga Taifa la Tanzania.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post