BARNABA: NISIFANANISHWE NA MTU

Elias Barnaba ‘Baba Steve’ .
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Elias Barnaba ‘Baba Steve’ amefunguka kuwa, kutokana na uwezo wa kimuziki alionao hakuna msanii yeyote Bongo anayeweza kufananishwa naye, licha ya kwamba wapo wengi wanaofanya vizuri.

Akizungumza na Mikito Nusunusu hivi karibuni, Barnaba alisema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kumjalia kipaji cha kipekee kwenye muziki na kwamba ataendelea kukitendea haki kwa kuwaburudisha wapenzi na wadau wa muziki kwa kiwango cha juu zaidi.

“Mimi ni mwanamuziki na si msanii, lazima kwanza utofautishe mambo hayo mawili, ndiyo maana ninaweza kutunga na kuimba na hata kutumia vyombo vyote vya muziki, hiyo ndiyo maana halisi ya mwanamuziki. Naomba sana nisifananishwe na mtu kwenye eneo hilo. Nilizaliwa kuburudisha watu na ninafanya muziki kama sehemu ya maisha yangu, siangalii fedha na masilahi, muziki uko kwenye damu,” alisema Barnaba.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post