BEKI MPYA WA MAN CITY AVUNJA REKODI YA DUNIA YA USAJILI, NI KYLE WALKER KUTOKA TOTTENHAM

Manchester City imekamilisha usajili  wa mlinzi Kyle walker kutoka Tottenham kwa kandarasi ya Pauni milioni 54  kukipiga Etihad  kwa miaka mitano.Kwa uhamisho huo, Walker anakua mlinzi ghali zaidi kununuliwa katika historia.
Mchezaji huyo alijiunga na Tottenham mwaka 2009 na kucheza michezo zaidi ya 200. Kwa wiki, Walker atajichukulia mshahara wa Pauni 130,000.
“Nafurahi kusaini na Manchester City, na nasubiri kwa hamu kuanza kuichezea”. Alisema Walker.

‘Pep Guardiola ni mojawapo wa makocha wanaoheshimika duniani na nafikiri atanisaidia kunipeleka mbele zaidi katika kucheza kwangu’

Walker ndiye mchezaji wa tatu kusainiwa na Manchester City katika dirisha hili la usajili, mbele ya Bernado Silva  kutoka Monaco na golikipa Ederson kutoka Benfica.

Guardiola alisema kuwa Walker ndiye chaguo lake la kwanza kwa mlinzi wa kulia, baada ya Zabaleta na Bacary Sagna kuondoka.

Dili hilo la pauni Milioni 54 limevunja rekodi ya dunia kwa mlinzi kusajiliwa kwa kiasi hicho cha fedha, wakala wake Base Soccer aliandika kupitia Twitter.

 David Luiz ndiye aliyekua anashikilia taji hilo, baada ya kusajiliwa na  Paris Saint-German kutoka Chelsea mwaka 2014 kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 50.

Pia, Walker anakua ndiye mchezaji ghali zaidi wa Kiingereza wa muda wote na kumpiku Raheem Sterling. 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post