BEKI WA AZAM FC AZIFAGILIA SIMBA, YANGA, ASEMA ZITATISHA MSIMU UJAO

Beki wa kati wa Azam FC, Agrrey Morris amesema anazipa nafasi kubwa klabu za Simba na Yanga kufanya vizuri kwenye ligi ya msimu ujao kutokana na usajili walioufanya kipindi hiki cha dirisha kubwa.
Morris amesema kinachomfanya aitoa Azam kwenye mbio za ubingwa ni kutokana na kuondokewa na idadi kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na wanaijia vizuri falsafa inayotumiwa na timu hiyo.
“Siwabezi wachezaji walisajiliwa kuziba nafasi za wale walioondoka, lakini niseme ukweli kwamba wachezaji wapya walioletwa watahitaji muda ili kuweza kuendana na mfumo wa timu lakini pia wale walioondoka walikuwa ni watu wenye uzoefu mkubwa ukilingananisha na hawa wapya,” amesema Morris.
Beki huyo aliyeipa mafanikio makubwa Azam tangu alipojiunga nayo misimu mitano iliyopita, amesema kikosi chao cha msimu ujao kinahitaji maandalizi ya kutosha ikiwemo wachezaji kucheza kwa kujitolea ili kupata matokeo ambayo wamekusudia kuyapata.
Amesema ushindani umebadilika kwa asilimia kubwa hivyo kama kweli wanataka kurudi kwenye nafasi za juu na kupata moja ya nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa lazima wapambane na kurudisha enzi ya nyuma ambapo kikosi chao kilikuwa na nyota kadhaa wakiwemo John Bocco , Kipre Tchetche na wengine.
Kipa Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael na Bocco wameondoka kwenye timu hiyo baada ya mikataba yao kumalizika na uongozi ulipotaka kuwaongezea walishindwa kuelewana katika maslahi.
Klabu za Simba Yanga na Azam kwasasa ndiyo zinapambana kwa kupigana vikumbo kusajili wachezaji ambao mabenchi yao ya ufundi wanaamini watawapa mafanikio.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post