BENDERA ZA CHADEMA ZAMPONZA MBUNGE WA MBOZI KATIKA ZIARA YA WAZIRI MKUU

Jeshi la Polisi lilimuita na kumhoji Mbunge wa Mbozi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Pascal Haonga kutokana na bendera za chama hicho kupepea kwa wingi katika mji wa Mlowo wilayani Mbozi.
Hatua ya mbunge huyo kuitwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange inakuja kufuatia bendera hizo kupeperushwa kwa wingi wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitarajia kuzungumza na wananchi wa eneo hilo katika mkutano wa hadhara.
Mbunge hiyo alithibitisha kuitwa na Polisi kufuatia eneo hilo lenye wafuasi wengi wa CHADEMA kupeperusha bendera. Alisema kuwa, alipigiwa simu na kamanda huyo na kutaka waonane Ikulu ndogo ya Mkoa wa Songwe.
Aidha, alisema alikwenda na kuonana na kamanda huyo, na walifikia makubaliano ya kutoondoa bendera hizo.
“Miongoni mwa mambo tuliyozungumza ni pamoja na kupandishwa kwa bendera za CHADEMA, katika Mji wa Mlowo, mazungumzo yameisha na hakuna bendera zitakazoshushwa,” alisema Haonga.
Chanzo: MTANZANIA
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post